Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif akimkabidhi zawadi Kipa Bora wa mashindano ya ujirani mwema
ya Dr. Sheni Cup yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM Jimbo la
Nungwi.
Balozi Seif akimkabidhi Kepteni wa Timu ya Soka ya Kitamli ya Nungwi Makame Mohd Haji jezi na vifaa baada ya timu hiyo kuibuka bingwa wa Dr. Sheni Cup huko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja
Balozi Seif akimkabidhi Kikombe Kepteni ya Mabanati wa Timu ya Pete ya Tusitengane ya Nungwi Ndamu Makame Mussa baada ya kuibuka na ushindi wa Kombe la Mwanamwema Sheni dhidi ya Timu ya Pete ya Tuko Imara.
Kepteni wa Timu ya Soka ya Kitamli ya
Nungwi Makame Mohd Haji akifuahia kikombe anachokabidhiwa na mgeni rasmi
balozi Seif baada ya kutawadhwa kuwa mabingwa wa kombe hilo.
Kati kati yao ni lezi wa Jimbo la Nungwi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa wa Idara Maalum Haji Omar Kheir.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif akizungumza na Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Michezo
Zanzibar { BTMZ } Sharifa Khamis hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar
katyika kubadilishana mawazo ya namna ya kufufua michezo ya ndani
inayoonekana mingi kufifia.
Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Michezo
Zanzibar { BTMZ } Sharifa Khamis akipokea mchango wa shilingi Milioni
2,000,000/- kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi kwa ajili ya kusaidia ufufuaji wa michezo ya ndani inayoonekana
kufifia hapa Nchini.
Picha na Hassan Issa wa – OPMR – ZNZ.
NA Othman Khamis Ame, OMPR
Hatimae Mabingwa wa
Mashindano ya Ujirani mwema ya Dr. Sheni Cup yaliyoandaliwa na Umoja wa
Vijana wa CCM Jimbo la Nungwi na kufadhiliwa na Rais wa Zanzibar Dr.
Ali Mohammed Sheni amepatikana katika mchezo wa Fainali ya mashindano
hayo yaliyozikutanisha Timu za Soka za Kitamli ya Nungwi dhidi ya
wapinzani wao Timu ya Soka ya Mwendo Mdundo ya Kidoti.
Pambano hilo la
Fainali lililoshuhudiwa na umati mkubwa wa wapenzi wa soka wa Jimbo la
Nungwi na Vitongoji vyake limeiwezesha Wenyeji wa mashindano hayo Timu
ya Kitamli ya Nungwi kuibuka na ushindi kwa kuilaza Mwendo Mdundo ya
Kidoti Goli 1-0.
Timu ya Kitamli
ilijipatia goli lake la pekee na la ushindi lililofungwa na mchezaji
Haji Wa Haji katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo ambapo mgeni
rasmi katika pambano hilo la Fainali ya Dr. Sheni Cup alikuwa Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Mashindano hayo ya
ujirani mwema yaliyoanza kutimua vumbi Tarehe 24/8/2013 yamejumuisha
Timu Tisa kutoka katika vijiji tofauti vya Jimbo la Nungwi yakienda
sambamba na yale ya mchezo wa Pete { Net Ball } kwa Wanawake
yaliyojumuisha Timu Nne.
Akizungumza mara baada
ya pambano hilo la Fainali Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif aliwahimiza Vijana hao kujitahidi kujifunza zaidi michezo ili
wajijengee njia rahisi ya kupata ajira kupitia sekta ya michezo ambayo
wakati huu imekuwa na thamani kubwa Duniani.
Balozi Seif alisema
Ulimwengu hivi sasa umeshuhudia ongezeko kubwa la ajira kupitia Sekta ya
michezo hasa Mchezo wa soka na Table Tennis ambayo imeonekana
kutajirisha wanamichezo wengi wenye vipaji vikubwa vya michezo hiyo.
“ Tumeshuhudia
wachezaji mbali mbali Duniani wakiwemo pia wale wanaotokea Bara letu la
Afrika wakicheza mpira wa kulipwa katika timu mbali mbali za bara la
Ulaya hasa ndani ya Uingereza. Huo ni Mfano halisi mmaopaswa kuutilia
maanani ili na nyinyi siku moja mjikute mmetinga katika vilabu hivyo
maarufu Duniani “. Alisisitiza Balozi Seif.
Mapema Mlezi wa Jimbo
la Numngwi ambae pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Idara Maalum Haji Omar Kheir alisema mashindano hayo yaliyoandaliwa na
Umoja wa Vijana wa CCM wa Jimbo hilo kwa ushauri wa Mke wa Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi ni utekelezaji wa Ilani
ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010.
Haji Omar alisema
ilani hiyo imeeleza umuhimu wa uimarisha michezo katika maeneo mbali
mbali nchini lengo likiwa kuwajengea afya njema pamoja na ajira
wananchi wanaoshiriki michezo hiyo.
Katika kuunga mkono
uendelevu wa mashindano hayo Waziri Haji Omar aliahidi kuchukuwa dhamana
ya malipo kwa deni linalodaiwa Kamati ya mashindano hayo linalohusu
malipo ya posho za waamuzi pamoja na baadhi ya vifaa vya mashindano
hayo.
Katika fainali hiyo
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikabidhi Kikombe kwa
Mabingwa wa Mashindano hayo Timu ya Kitamli ya Nungwi, Jezi, Mpira
pamoja na Shilingi laki 300,000/-.
Balozi Seif pia
alimkabidhi mshindi wa pili Mwendo Mdundo ya Kidoti Jezi, Mpira na
Shilingi Laki 150,000/- wakati mshindi wa Tatu Timu ya Mapinduzi ya
Kidagoni ikakabidhiwa Jezi, Mpira na Shilingi 75,000/-.
Baadae Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar akakabidhi shilingi 50,000/- kwa kila Timu bora ,
Mchezaji bora, mfungaji bora, Muamuzi bora, Mchezaji mdogo kuliko
wote,kipa bora pamoja na kocha bora kwenye mashindano hayo.
Mashindano hayo
yaliyopewa jina la Dr. Sheni Cup kwa mchezo wa Soka na Mwanamwema Sheni
Cup kwa mchezo wa Pete { Net Ball } yamegharimu jumla ya shilingi
milioni Sita Nukta Tano { 6,500,000/- }.
Wakati huo huo Makamu
wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikabidhi mchango wa shilingi
Milioni 2,000,000/- kwa ajili ya kusaidia ufufuaji wa michezo ya ndani {
Indo games } hapa Nchini ambayo mingi inaonekana kufifia na mengije
kufa kabisa kwa kipindi kirefu sasa.
Akikabidhi mchango huo
kwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar { BTMZ } Sharifa
Khamis hapo Ofisini kwake vuga Mjini Zanzibar Balozi Seif alisema
Zanzibar ilikuwa ikisifika kimataifa kwa michezo ya ndani sifa ambayo
hivi sasa imekufa kutokana na kufifia kwa michezo hiyo.
Alisema juhudi za
pamoja zinahitajika kuchukuliwa katika kuona michezo hiyo inachipuka
tena hapa Nchini kwa kuwapa nguvu za uwezeshaji na vifaa wachezaji
wanaojihusisha na michezo hiyo.
“ Vijana lazima
waendeleze pia michezo ya ndani kama vile Table Tennis, Vinyoya, Beach
Ball, Triatholon na riadha badala ya kuelekezaa nguvu zao zaidi kwenye
soka ili kurejesha sifa hiyo Kimataifa “. Alisisitiza Balozi Seif.
Akipokea mchango huo
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar { BTMZ }
Sharifa Khamis { Sherry } alisema msaada huo wa Balozi Seif ni hatua ya
awali katika kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Taasisi za Michezo
Nchini katika kufufua vuguvugu la michezo hapa Nchini.
Mwenyekiti Sharifa {
Sherry } alisema katika kwenda samba mba na ufufuaji huo Baraza la Taifa
la Michezo Zanzibar kwa kushirikiana na Chama cha Soka Zanzibar {
ZFA } hivi karibuni vinatarajiwa kufungua vuguvugu la michezo katika
kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
No comments:
Post a Comment