KUTOKA ZANZIBAR
Kikosi cha Zimamoto Zanzibar Chafanikiwa kuuzima Moto uliokuwa Unaunguza Nyumba ya Wanafunzi wa Al Haramyn
Askari wa Kikosi cha Zimamoto Zanzibar wakiwa katika zoezi ya kuuzima
moto uliokuwa ukiwaka katika Nyumba ya Dahaliya ya Wanawake ya Al
Haraymn Mpendae baada ya kutokea hitilafu ya umeme na kuteketeza karibu
malizote za Wanafunzi wanaoishi katika Nyumba hiyo leo mchana, katika
ajali hiyo hakuna Mwanafunzi aliyejeruhiwa katika moto huo.
Askari wa Kikosi cha Zimamoto wakiwa katika jitihada za kuuzima moto
uliokuwa ukiwaka katika Nyumba ya Dahaliya ya Wanawake ya Skuli ya Al
Rahamny Mpendae, Chanzo cha moto huo hakijajulikana.zaidi ya
mali za shilingi milioni 100 zimeteketea ikiwemo nyumba yenyewe
kuharibika vibaya kutokana na moto huo.
Wananchi wakiwa eneo la tukio katika mitaa ya Mpendae kwa mchina wakati nyumba hiyo ikiwa moto.
Askari wa Zima moto wakiwa katika zoezi hilo la kuzima moto huo.
Hivi ndivyoilivyoharibika nyumba hiyo baada ya kuungua kwa moto chanzo
chake hakijajulikana, na hakuna mwanafunzi aliyejeruhiwa katika ajali
hiyo ya moto.
Mmmoja wa Mwanafunzi aliyekuwemo katika dahaliya hiyo wakati ikiwa moto
na kuwahi kutolewa akiwa amelala akisaidiwa na Mwalimu wa Skuli hiyo,
Dahaliya hiyo inakadiriwa kuwa na Wanafunzi 25 wa Skuli ya Al Haramyn
wanaishi, wakati wa tukio baadhi ya wanafunzi walikuwa wamejipumzisha na
huku moto unawaka na kuokolewa na Wananchi na Walimu wa skuli hiyo
waliowahi kutowa msaada kabla ya kufika kwa Kikosi cha Zimamoto na
kuendelea kuuzima moto huo.
Baadhi ya Vitu vilivyookolewa katika nyumba hiyo ya Wanafunzi baadhi yake vikiwa vimeunguwa no moto huo.
Afisa wa Kikosi cha Zimamoto Zanzibar akizungumza na waandishi wa
habari waliofika eneo la tukio wakati wa zoezi la kuzima moto huo.
Mfanyakazi wa Skuli hiyo akizungumza na Waandishi wa habari kutokana na
tukio hilo la moto lililoikumba moja ya jengo la kuishi wanafunzi wa
skuli hiyo.
No comments:
Post a Comment