Thursday, September 05, 2013

PICHA NA MAELEZO ZAIDI YA MNIGERIA ALIYE KA MATWA NA MADAWA YA KULEVYA.

MNIGERIA ANASWA NA KETE 99 ZA MADAWA YA KULEVYA JNIA.

 
Anthonia Ojo (25) akitoa madawa ya kulevya katika makopo ya poda na shampoo baada ya kukamatwa.
 
Mzigo aliodakwa nao Anthonia Ojo huu hapa.
 
Mtuhumiwa huyu hapa.
 
Begi alipokuwa ameweka mzigo huo.

-ALIKUWA AKIELEKEA ITALIA KUPITIA UFARANSA
-ALIYAFICHA KATIKA MAKOPO YA PODA NA SHAMPOO
-ADAI KUYANUNUA MAGOMENI
-UCHUNGUZI UKIBAINIKA ATAPANDISHWA KIZIMBANI

Jitihada za kurejesha heshima kwa viwanja vya ndege nchini zilizo anzishwa na waziri wa uchukuzu Dk. Harisson Mwakyembe zinaonekana kuzaa matunda baada ya mwana dada kutoka nchini Nigeria Anthonia Ojo (25) kukamatwa na kete 99 za madawa ya kulevya Uwanja wa Ndege wa Dar es salaam Jana.
 
Mwanamke  huyo amekamatwa  akieleke Roma Italia kupitia Paris Ufaransa kwa ndege ya Ethiopian Airways  na  aliingia hapa nchini Agosti 30 akitokea Nigeria. 

na baada ya kuhojiwa alidai kuwa dawa hizo alizinunua maeneo ya Magomeni, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Viwanja vya Ndege, Renatus Chalya, Ojo ataendelea kubaki chini ya ulinzi wa polisi kwa uchunguzi zaidi, wakati madawa hayo yamepelekwa kwenye  ofisi ya mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini aina ya dawa hizo  na   thamani yake.


 
Passport ya Ojo.
 
Ojo akishushwa kwenye gari baada ya kukamatwa.
 
Mikononi mwa polisi.
 
Madawa aliyokamatwa  nayo Ojo baada ya kutolewa kwenye makopo.

No comments:

Post a Comment