Tuesday, September 03, 2013

Picha zaidi za Kongamano la  Kimataifa la Historia ya Ustaarabu wa Uislam Zanzibar.

 
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza wakati alipolifungua Kongamo la Kimataifa la siku tatu kuhusu historia ya ustaarabu wa Kiislamu katika Afrika ya Mashariki huko katika Ukumbi wa Hoteli ya Lagema Mkoa wa Kaskazini Unguja,(kulia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna,na Dkt. Abdul Muneium Al-Hasni, Waziri wa Habari wa Falme ya Oman 
    Wajumbe wa Mkutano wa Kimataifa wa Kongamano la Historia ya Ustaarabu wa Kiislam wakimsikiliza Mgeni Rasmin Rais wa Zanzibar akifungua Kongamano hilo.
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamuhuna, akihutubia katika Kongamano hilo na kumkaribisha Mgeni Rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Ali Mohamed Shein, kufungua Kongamano hilo katika ukumbi wa hoteli ya Lagema Zanzibar.
Balozi wa Oman Nchini Tanzania Balozi Yussuf Ak Bakry, akitowa salamub za Nchi yake katika Ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Historia ya Ustaarabu wa Uislam, katika ufunguzi wa Kongamano hilo katika ukumbi wa hoteli ya Lagema Nungwi Zanzibar
Dkt. Hamad Bin Mohammed Al Dhawyan,akisoma risala kwa Niaba ya Mwenyekiti wa Mamlaka ya Nyaraka za Kumbukumbu za Oman., katika Ufunguzi wa Kongamano la MKimataifa la Historian a Ustarabu wa Kiislam, lililoandaliwa na Serekali ya Mapinduzi Zanzibar, Serekali ya Oman na Uturuki, katika hoteli ya Lagema Nungwi Zanzibar.

Waalikwa katika Kongamano la Kimataifa la Historia ya Ustaarabu wa Kiislam wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akifungua Kongamano hilo la siku tatu.linalifanyika katika ukumbi wa hoteli ya lagema nungwi Zanzibar.
Makamo Mkuu wa Chuu Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA Profesa Idris Rai, akihutubia katika Kongamano hilo wakati wa Ufunguzi wake uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, na kusemaKongamano hili litaitangaza Zanzibar na Chuo Kikuu cha SUZA.kupitia Kongamano hilo.
Washiriki wa Kongamano wakifuatilia Mada zinazowakilishwa katika Kongamano hilo la Kimataifa.
//// Katibu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Waislam OIC Dkt. Ekmeleddin Ihsanoglu. Akitowa Salamu za OIC katika Kongamano hilo la Historia ya Utamaduni wa Uislam, lililofanyika katika Hoteli ya Lagema Nungwi Wilaya ya Kaskazini A Unguja.

JAJI Mkuu wa Zanzibar Omar Makungu akitowa Mada ya Historia ya Mahakama ya Kadhi Zanzibar kuazishwa kwake hadi leo, katika Kongamano hilo lililofanyika Zanzibar katika hoteli ya Lagema Nungwi Zanzibar.
Mtoa Mada kutoka Burundi Dkt. Mohammed Rukara Halfan, akitowa Mada kuhusu Jukumu la Oman katika kusambaza Utamaduni wa Kiislam katika Nchi za Afrika Mashariki.

Washiriki wa Kongamani wakiwa ukumbi wa mkutano wakifuatilia mada zinazowakilishwa na Wahadhiri wa Vyuo Vikuu, jumla ya mada 62 zitawakilishwa katika Kongamano hilo.
Viongozi wa meza Kuu wakifuatilia Mada katika Kongamano hilo katika ukumbi wa hoteli ya Lagema Zanzibar Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Wajumbe wa Kongamano la Kimataifa la Historia na Ustaarabu wa Kiislam wakimsikiliza mtowa Mada katika Kongamano hilo lililofanyika Hoteli ya Lagema Nungwi.Wilaya ya Kaskazini A Unguja.

No comments:

Post a Comment