Karibuni wapenzi wa makala haya ya afya, natumaini mnaendelea kujifunza kupitia safu hii.
Leo tunazungumzia ugonjwa unaosumbua sana jamii yetu wa anemia au sickle cell.
Anemia au sickle cell ni hali ambayo huwakuta watu wenye upungufu wa chembechembe nyekundu kwenye damu. Maana yake ni kwamba miili yao huwa haibebi hewa ya kutosha ya oksigeni. Hali hii inaweza kuwafanya wawe wagonjwa.
Ugonjwa mara nyingi ni wa kurithi. Mtu huupata kutoka kwa wazazi wake. Kila mtu hupata nusu ya jeni (genes) zake kutoka kwa mzazi wa kiume nusu na kutoka kwa mzazi wa kike. Iwapo wazazi wote (baba na mama) wana jeni ya sickle cell, wanaweza kupata mtoto aliye na ugonjwa huu hata kama wao wenyewe hawana.
Dalili
Dalili za kuwa na maradhi haya ni homa, maumivu ya kifua, kupumua harakaharaka, uchovu, kuvimba kwa tumbo au sehemu za chini yake, kupoteza nguvu na macho kukosa nuru ya kuona vizuri.
Tiba na ushauri
Ukiona dalili kama hizi zinakutokea mara kwa mara muone daktari mara moja ambaye atakupima damu yako kubainisha iwapo una huo ugonjwa na atakupa matibabu.
Daktari wako atakupa ushauri, atakupatia dawa pia atakupa ushauri wa vyakula ambavo utakuwa ukitumia hasa mboga za majani kwa wingi,samaki,dagaa maziwa na matunda ambayo yatakusaidia kwa kiasi ili tatizo hilo lisikudhuru kwa kiasi kikubwa.
Wapo watu wanaishi muda mrefu bila kusumbuliwa na tatizo la kupungukiwa na damu kwa sababu wanazingatia masharti.
Ugonjwa wa upungufu wa damu mwilini ni hatari sana hivyo inapaswa wanaosumbuliwa na maradhi hayo kuzingatia masharti ikiwa ni pamoja na kula vyakula vinavyoongeza damu hasa mboga za majani.
Aidha, watumie dawa za kuongeza damu watakazoshauriwa na madaktari wao.
No comments:
Post a Comment