Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua Uwanja wa ndani wa
michezo katika Chuo Cha michezo huko Malya,Wilayani Kwimba,Mkoani Mwanza
leo.Wengine katika picha ni Waziri wa Habari na michezo Dkt.Fenela
Mkangara(wapili kushoto),Mbunge wa Sumve Richard Ndassa(wanne
kulia),Mbunge wa Kwimba Mhe.Mansour na kushoto ni Mkuu wa Chuo Cha
Michezo Malya Bwana Allen Alex
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Pereira Silima
wakifunua kitambaa wakati wa uzinduzi wa kituo Kikuu cha Polisi
Wilayani Kimba Jana.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereira
Silima(kushoto),Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo(watu
kushoto) na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ernest Mangu(kulia)
wakikata utepe kuzindua rasmi Kituo Kikuu cha Polisi Ngudu,Wilayani
Kwimba Jana.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa cheti Dkt.Makori Josephat Maro(picha
ya juu kabisa) na Nesi Rhoda Joseph Michael(pichani juu) kwa kutambua
kitendo cha ujasiri wa wahudumu hao wa sekta ya Afya kuokoa maisha ya
mama mjamzito na mwanaye mchanga kwa kumuongezea damu yao wenyewe na
kumuwezesha kujifungua salama.Mama huyo akiwa mjamzito alifika
hospitalini hapo peke yake akiwa na damu pungufu.Baada ya kukosa ndugu
wenye damu inayoendana na damu ya mama huyo wahudumu hao walijitolea
damu na kumuwezesha mama huyo kujifungua salama katika hospitali ya
Wilaya ya Kwimba.Mbali na vyeti uongozi wa wilaya ya Kwimba uliwazawadia
shilingi laki tano kila mmoja.Baada ya kuguswa na kitendo hicho Rais
Dkt.Jakaya Kikwete aliwazawadia Dkt.Makori maro na Nesi Rodha Michael
shilingi milioni moja na nusu.
picha na( Freddy Maro)
No comments:
Post a Comment