Tuesday, September 10, 2013

UJUMBE MAALUM


Asalaam Alaykum Ndugu zangu wapendwa Asubuhi Njema Naomba Tukumbushane hili Serikali ilipotoa wito kwa Watu wasio na Vabali Maalum vya Kuishi Nchini haina Maana kwamba Wananchi tumepewa Ruhsa ya Kunyanyasa kila Mgeni ambaye una Mdhania hana Kibali kwa Kumpora Mali zake na Kumpiga N.K

Ukifanya tendo hilo la kumnyanyasa Mtu na kumpiga kuchukua Mali zake Kisa eti hana Kibali cha kuishi utakuwa Umemkosea M/Mungu kwa Tendo lako na M/Mungu atakulipa Malipo yanayo stahili na Kitendo chako sababu hao nao ni Binaadamu ambao wana stahili kila aina ya Ubinaadamu na kulindiwa Mali zao walizo tafuta kwa Jasho lao.

Tukumbuke kuwa Sio WAO TU WAPO TANZANIA KINYUME CHA SHERIA HATA NDUGU ZENU WENGI WAPO NJE ZA NCHI KINYUME NA SHERIA HIVYO.

Hivyo Mkianza Sisi tutamaliziwa Tuendeleze Ustaarabu wetu wa KIDINI NA KIZALENDO KATIKA KUISHI NA WATU KI WEMA IKIWA UNA DHANI KUWA FULANI NI KATIKA WAHAMIAJI  AMBAO WAPO KINYUME NA SHERIA NA UNATAKA ISAIDIA SERIKALI TOA TAARIFA KATIKA VYOMBO HUSIKA NA SIO KUFANYA VITENDO VISIVYO KUWA VYA KI - BINAADAMU.

SHUKRAN KWA KUSOMA KWAKO UJUMBE HUU.

No comments:

Post a Comment