Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mamia ya wakazi wa Wilaya ya Magu,Mkoani Mwanza jana mchana.
Mamia
ya Wakazi wa Wilaya ya Magu wamkimsikiliza Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete wakati alipowahutubia katika mkutano wa hadhara mjini Magu jana
Rais
Jakaya Kikwete akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Magu Mheshimiwa
Jaqueline Liana, (kushoto,) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist
Ndikilo (katikati) mara baada ya kuwasiri katika makao makuu ya kata ya
Lugeye ambako kulitolewa taarifa ya wilaya ya Magu
Rais
Jakaya Kikwete akiangalia ngoma ya wananchi wa kabila la Wasukuma
wanayocheza na nyoka aina ya chatu wakati wa sherehe za ufunguzi wa
jengo la zahanati ya Lugeye iliyopo wilayani Magu. Zahanati hiyo
imegharimu kiasi cha milioni 170.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi jengo la zahanati ya Kata ya Lugeye huko wilayani Magu t
Rais
Jakaya Kikwete akisalimiana na Kanali Mstaafu wa Jeshi, Shadrack
Faustino Mbilizi aliyehudhuria sherehe za ufunguzi wa jengo la zahanati
ya Lugeye huko Magu na pia alipokea kupokea kadi yake ya kitambulisho
cha matibabu kwa wazee .
Rais
Jakaya Kikwete akipokea kitambulisho cha matibabu kwa wazee kutoka kwa
Mkuu wa Wilaya ya Magu Mheshimiwa Jaqueline Liana kwa ajili ya kupewa
Kanali Mstaafu Shadrack Mbilizi na mkewe Mariam Said wakati wa sherehe
za ufunguzi wa jengo la zahanati ya Lugeye
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi wa kata ya Lugeye wakati wa sherehe za kufungua jengo la zahanati ya kata hiy
Rais
Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya Mkurugenzi
Mtendaji wa Wilaya ya Magu eneo la Ilungu karibu na mji wa Magu. Jengo
hilo litagharimu shilingi bilioni 6 na milioni 700 litakapokamilika.
Rais
Jakaya Kikwete ngoma ya utamaduni wilaya ya Magu kabla ya kuhutubia
mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha sabasaba mjini Magu
Rais
Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa wilaya ya Magu kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha sabasaba mjini Magu. Picha
zote na John Lukuwi
No comments:
Post a Comment