Tuesday, September 03, 2013

Dk Shein azindua Kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu historia ya ustaarabu wa Kiislamu katika Afrika ya Mashariki

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN ASHIRIKI KONGAMANO LA KIISLAMU

IMG_3682  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza wakati alipolifungua Kongamo la Kimataifa la siku tatu kuhusu historia ya ustaarabu wa Kiislamu katika Afrika ya Mashariki huko katika Ukumbi wa Hoteli ya Lagema Mkoa wa Kaskazini Unguja,(kulia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna,na Dkt. Abdul Muneium Al-Hasni, Waziri wa Habari wa Falme ya Oman.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_3617 
Baadhi ya waalikwa katika Kongamo la Kimataifa kuhusu historia ya ustaarabu wa Kiislamu katika Afrika ya Mashariki,
litakalofanyika kwa muda siku tatu huko katika Ukumbi wa Hoteli ya Lagema Mkoa wa Kaskazini Unguja,wakifuatilia kwa makini mada zilizotolewa katika Mjadala huo ulioanza leo. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_3716  
Baadhi ya Viongozi walioalikwa katikaKongamano la Kimataifa kuhusi Historia ya Ustaarabu wa Kiislamu katika Afrika ya Mashariki,wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akilifungua kwa kutoa hutuba yake,katika ukumbi wa Lagema Hotel Mkoa wa Kaskazini Unguja.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_3823 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa kulifungua Kongamano la Kimataifa la kuhusu historia ya ustaarabu wa Kiislamu katika Afrika ya Mashariki, (wa pili kulia) Dkt. Abdul Muneium Al-Hasni,Waziri wa Habari wa Falme ya Oman,Dkt. Emeleddin Ihsan,Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu Duniani (OIC);na Dkt. Hamad Mohamed Al-Dhawiani, Mwenyekiti  wa Mamlaka ya Kumbukumbu na Nyaraka ya  Falme ya Oman, [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

No comments:

Post a Comment