Awali
ya yote nashukuru kupata fursa hii ya kukutana na vyombo vya habari ili
kuzungumizia baadhi tu ya mafanikio ambayo Hospitali ya Taifa Muhimbili
imeyapata kupitia Kituo cha Upasuaji Moyo na Mafunzo (Cardiac Surgery
Treatment and Training Centre.
Huduma za Upasuaji Moyo:
Kama
mnakumbuka tarehe 21 Mei 2008 upasuaji wa moyo ulianza rasmi hapa
Muhimbili, ukifanywa na madaktari wetu baada ya kupata mafunzo nchini
India na Israel. Wagonjwa 105 walifanyiwa upasuaji katika kipindi cha
mwaka mmoja na hadi kufikia leo tayari wagonjwa 453 wameshafanyiwa
upasuaji. Upasuaji wa moyo unaofanyika ni sawa na upasuaji katika vituo
vikubwa vya upasuaji wa moyo duniani kote. Wataalam wetu wamekuwa
wakifanya upasuaji wa kuziba matundu kwenye moyo na kubadilisha valvu
ambazo zimebana na kushindwa kuruhusu damu kupita kwenye moyo au kulegea
na kufanya damu kuvuja kwenda kwenye sehemu isiyohusika katika moyo na
kurudisha moyo katika hali yake ya kawaida ya afya ya mgonjwa.
Pamoja na kufanya upasuaji huduma nyingine ambazo zimefanyika na zinaendelea kufanyika ni pamoja na kliniki
mbalimbali kama vile za magonjwa ya valve, moyo kupanuka, mishipa ya
moyo kuziba, mapigo ya moyo kushuka, magonjwa ya moyo ya kuzaliwa ya
watoto na upasuaji wa moyo na mishipa ya damu.
Ufungaji wa Vifaa Tiba:
Kituo
hiki kina vifaa vya kisasa na vya hali ya juu na mahsusi kwa ajili ya
kumudu matibabu ya magonjwa makubwa ya moyo. Hospitali inaendelea
kutafuta taasisi zenye uzoefu mkubwa wa matibabu ya moyo ili kuanzisha
ushirikiano utakaowezesha kupata wataalamu wao kuja kushirikiana na
wataalamu wetu kutibu magonjwa makubwa ya moyo hapa hapa nchini kama
njia ya kuongeza uwezo kitaaluma. Tunafurahi kuwaambia kuwa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii imetoa fedha kwa ajili ya kununua mtambo mkubwa wa kuchunguza
mishipa na shinikizo ndani ya moyo na maradhi makubwa ya moyo ya
kuzaliwa (Catheterization Laboratory). Huu ndiyo mtambo amboa kwa
kipindi kirefu umekuwa ukipelekea Serikali yetu kupeleka wagonjwa wengi
wa moyo kufanyiwa matibabu nchini India. Mtambo huu umefungwa siku za
hivi karibuni, tutaujaribu (testing) mapema mwezi Oktoba mwaka huu. Mtambo huu umeigharimu Serikali kiasi cha shilingi bilioni 3.6
Jinsi mtambo wa (Catheterization Laboratory) unavyofanya kazi:
Mtamo
huu wa Cath Lab ndio unaotusaidia kuangalia mishipa ya damu inayoenda
kwenye moyo, kuangalia moyo jinsi unavyofanya kazi na pia kama mtu
anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo mashine au mtambo huu unatusaidia
kuangalia vitu mbalimbali kwenye moyo wa mgonjwa husika ili kujiridhisha
kuona kama kuna jinsi yoyote mgonjwa huyu atanufaika na upasuaji huu.
Cath Lab inasaidia pia kuweka kifaa saidizi katika moyo wa mtu
(pacemaker) ambacho ni kama betri kinachosaidia kuufanya moyo ufanye
vizuri siku zote.
Wafanyakazi wa Kituo hiki:
Kituo
hiki kinahitaji wafanyakazi wa kada mbalimbali wapatao 365 lakini kwa
sasa kina watalaam 121. Lakini nafurahi kuwambia kuwa katika mwaka
uliopita wa fedha tulipata kibali kwa ajili ya kuajiri wafanyakazi zaidi
ya 100 ili kukidhi mahitaji halisi ya kituo hiki katika kutoa huduma. Pamoja
na hayo tuna changamoto ya kupata watalaam waliobobea katika magonjwa
ya moyo ambao hawapatikani kwa urahisi katika soko la ajira. Lakini
tunajithaidi kuajiri watalaam ambao tutawapeleka kubobea hususani katika
ubingwa wa nusu kaputi, upasuaji na mishipa ya damu, upasuaji wa moyo
kwa watoto n.k
Gharama za Matibabu:
Kama
mnavyojua, huduma za maradhi ya moyo zina gharama kubwa na zinahitaji
wataalamu wa hali ya juu. Ili huduma hii iwe endelevu, Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii inapitia upya utaratibu wa kulipia matibabu ikiwa ni na
kuzishauri kampuni zote za Bima ya Afya kulipia wateja wao wanaohitaji
huduma mbalimbali za moyo. Kwa kufanya hivyo Kituo kitaweza kujiingizia
kipato kitakachotumika kuboresha huduma pamoja na kuweka motisha kwa
wafanyakazi.
Kituo
hiki kitakuwa faraja kubwa kwa nchi yetu na kitaipunguzia Serikali
mzigo ikizingatiwa kwamba asilimia 70 kati ya wagonjwa wote wanaopata
rufaa ya Serikali kwenda kutibiwa nje ya nchi ni wagonjwa wa moyo. Mathalan
serikali kwa makisio inatumia kama dola za kimerakani 10,000 kulipia
gharama za matibabu ya mgojwa mmoja nje ya nchi ukilinganisha na dola
za marekani 6,000 mgonjwa akitibiwa katika kituo chetu cha Moyo
Kwa hiyo, kuanzishwa kwa kituo hiki kutapunguza matumizi ya Serikali
kwa kiwango kikubwa sana. Hata hivyo Serikali inapitia mchakato wa
uboreshaji wa utoaji wa huduma pamoja na upatikanaji wa fedha ili kila
Mtanzania aweze kupata huduma bora hapa kwetu.
Uwekezaji Uliofanywa hadi sasa
Ujenzi
wa Kituo hiki umejengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China. Ujenzi pamoja ufungaji wa vifaa
hadi hivi sasa umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 32 ambapo Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechangia kiais cha shilingi bilioni
16,411,741,367 ambapo Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imechangia
shilingi bilioni 15,630,769,600. Uwekezaji huu ni wa dhati na tuna kila
sababu ya kuipoingeza Serikali zote mbili kwa kazi kubwa iliyofanyika
hapa.
Mchanganuo wa uwekezaji umebainishwa katika jedwali lifuatalo;
Na
|
Maelezo
|
Bei kwa Tshs
|
1
|
Msaada wa Ujenzi na kufunga baadhi ya vifaa kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China
|
15,630,769,600.00
|
2
|
Mchango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya ujenzi
|
1,900,000,000.00
|
3
|
Bajeti
ya Maendeleo kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
ajili ya kununua vifaa tiba, mitambo na ufungaji katika kipindi cha
2010 – 2013
|
11,974,000,000.00
|
4
|
Gharama za Uendeshaji kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
toka mwaka 2008 – 2012
|
3,400,723,973.00
|
|
Jumla Kuu
|
32,905,493,573.00
|
Utaratibu wa Kutibiwa katika Kituo hiki:
Kituo
hiki cha Mafunzo na Upasuaji wa Moyo kitapokea wagonjwa kupitia mfumo
wa rufaa kwa Hospitali zote zilizothibitishwa kuleta wagonjwa Hospitali
ya Taifa Muhimbili ambapo kundi la kwanza ni Hospitali zilizoko katika
Jiji la Dar es Salaam ambazo ni CCBRT,
Lugalo, Amana, Temeke, Mwananyamala, Hospitali binafsi kama Agha Khan,
Hindu Mandal, Kairuki n.k. aidha tutapokea wagonjwa kutoka Hospitali za
Rufaa ngazi ya Kanda kama KCMC, Bugando, Mbeya na Hospitali zote za
Mikoa, Wilaya na Hospitali Teule.
Tumeweka wagonjwa katika makundi matatu yafuatayo;
Wagonjwa wa Msamaha
Kutokana
na Sera ya Msamaha wagonjwa kwa njia hii watachujwa ili kuhakikisha
hakuna matumizi mabaya ya sera hii. Aidha tunaweka utaraitibu mzuri wa
kuiomba Serikali kulipa fedha zote kwa Hospitali kwa wagonjwa wote
watakaopewa huduma kwa njia ya msamaha.
Uchangiaji wa gharama za matibabu
Hapa
ndugu na wanafamilia wa mgonjwa kama ilivyokawaida watatakiwa kuchangia
gharama za matibabu ambapo kiasi kingine kitalipwa na Serikali kuu au
Serikali za Mitaa kulingana na mgonjwa alikotoka.
Wagonjwa wa Kulipia (Private)
Kundi
hili ni kwa wateja ambao wana uwezo wa kulipia fedha taslimu au kupitia
bima za afya mbalimbali ambazo zipo kwa sasa. Baada ya kusema hayo
nawashukuruni sana kwa kunisikiliza.
Asanteni
Dkt. Marina Njelekela,
MKURUGENZI MTENDAJI,
SEPTEMBA 9, 2013.
No comments:
Post a Comment