Monday, September 09, 2013

TAARIFA KWA WANANCHI KUHUSU UBORESHAJI WA HUDUMA MAGONJWA YA MOYO HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI SEPTEMBA 9, 2013

Pix 0 

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uboreshaji wa huduma za magonjwa ya moyo katika hospitali ya taifa muhimbili, kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Zamaradi Kawawa. Pix 1 

Mkuu wa Kitengo Cha Moyo toka  Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Robert Mvungi akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) sababu za tatizo la ugonjwa wa moyo katika jamii. Pix 2 

Mkuu wa Kitengo Cha Moyo toka  Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Robert Mvungi akiwaonesha  waandishi wa habari (hawapo pichani) mchoro unaoonesha matundu katika moyo. Pix 3 

Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Agnes Kuhenga (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya gharama za matibabu katika kitengo cha magonjwa ya moyo katika hospitali ya Taifa Muhimbili, katikati ni Mkuu wa Kitengo hicho Dkt. Robert Mvungi na wa mwisho kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela Pix 4 
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela akiwaonesha waandishi wa habari moja ya chumba cha kupumzika wagonjwa mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo. Pix 5 

Mkuu wa Kitengo Cha Moyo toka  Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Robert Mvungi akiwaonesha  waandishi wa habari mtambo wa Cath Lab unaosaidia kuangalia mishipa ya damu inayokwenda kwenye moyo.
Picha Zote na Eliphace Marwa (MAELEZO)

No comments:

Post a Comment