Msemaji
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Erick Komba
akiongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano uliopo
makao makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam kuhusu ushiriki wa
Tanzania katika operesheni ya ulinzi na amani katika nchi ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC). Tanzania ni moja kati ya nchi tatu
zilizopeleka kikosi chake nchini DRC ikiwa ni sehemu ya SADC standby
brigade inayotoa mchango wake katika Jeshi la Umoja wa Mataifa (MONUSCO)
na kinafanya kazi chini ya Force Commander huku majukumu yake yakiwa ni
kuzuia waasi kujitanua, kuvunja nguvu ya waasi na kuwapokonya silaha
makundi yote ya waasi. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo)
Assah Mwambene.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (Maelezo) Assah Mwambene akiongea na waandishi wa
habari jinsi baadhi ya vyombo vya habari vinavyoandika taarifa
zisizo sahihi kuhusu ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika
operesheni ya ulinzi na amani katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC) ikiwa ni sehemu ya SADC standby brigade inayotoa mchango
wake katika Jeshi la Umoja wa Mataifa (MONUSCO) . Kushoto ni Msemaji wa
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Erick Komba.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (Maelezo) Assah Mwambene (kulia) akimuonyesha kitu
Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Erick
Komba wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo katika
ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya JWTZ jijini Dar es
Salaam. Mkutano huo uliongelea juu ya ushiriki wa Tanzania katika
operesheni ya ulinzi na amani katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC).
Mwandishi
wa Habari na Mpiga picha Mwandamizi wa kituo cha Televisheni cha
channel 10 Kibwana Dachi akiuliza maswali wakati wa mkutano
uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) jijini Dar es Salaam. Mkutano huo
uliongelea juu ya ushiriki wa Tanzania katika operesheni ya ulinzi na
amani katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(DRC). Wanaomsikiliza kwa makini ni Msemaji wa JWTZ Meja Erick Komba
(kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Assah
Mwambene(kulia).
Na Lorietha Laurence-Maelezo
JESHI
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limetoa taarifa ya maendeleo
ya wanajeshi wanaoshiriki kulinda amani kwa nchi mwanachama wa maziwa
makuu Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo eneo la Goma.
Taarifa
hiyo imetolewa na msemaji wa Jeshi hilo Meja Erick Komba alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Meja
Komba alisema kuwa baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya Kijamii
hususan “blogs” kuandika taarifa zisizo rasmi ambazo zinapotosha umma
kuhusu ushiriki wa Jeshi la Tanzania katika nchi ya Kongo.
Alieleza
kuwa jeshi la Tanzania linashiriki kulinda amani Nchini Kongo
kutokana na Rais wa nchi hiyo Mhe.Joseph Kabila kuwasilisha ombi katika
kikao cha nchi za maziwa makuu kilichofanyika Julai 12 mwaka jana
mjini Addis Ababa, Ethiopia baada ya waasi wa M23 kujitenga na Serikali
na kuanzisha mapambano.
“Ushiriki
wa Jeshi la Tanzania katika kulinda amani nchini Kongo umetokana na
ombi liliwasilishwa na Rais Mhe. Joseph Kabila kwa nchi wanachama wa
maziwa makuu ambazo ni Rwanda,Uganda,Tanzania na DRC kusaidia kulinda
amani na kuwapokonya waasi wa M23 silaha”alisema Meja Komba .
Meja
Komba aliongeza kuwa, jeshi la Tanzania ni sehemu ya SADC Standby
brigade iliyotoa mchango wake katika jeshi la Umoja wa Mataifa
(MUNUSCO) kinachofanya kazi chini ya “Force Commonder” ambapo majukumu
yake makubwa ni kuzuia waasi kujitanua, kuvunja nguvu za waasi na
kuwapokonya silaha makundi yote ya waasi.
Naye
Msemaji wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo
Bw. Assah aliwaomba waandishi na wadau mbalimbali wa habari kuandika
habari zenye uhakika na ambazo hazitapotosha umma.
“Nawaomba
waandishi na wadau wa habari tuwe tunatoa taarifa zilizo sahihi ili
tusipotoshe umma ukizingatia jeshi letu lipo huko kwa ajili ya kulinda
amani na siyo kupigana na M23,” alisema Mwambene.
Jeshi
la Ulinzi la Wananchi Kikosi cha Tanzania kiko chini ya MUNUSCO ambao
ndio wanaoendesha operasheni ya kulinda amani na Tanzania haipigani
na M23 wala haina tatizo na Rwanda kuhusiana na operesheni hiyo.
Pia Rwanda imesaidia Tanzania kwa kuruhusu kikosi kupitisha watu, vifaa na zana kuelekea Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
No comments:
Post a Comment