Mkuu
wa Jeshi la Polisi, IGP Saidi Mwema akionyesha ngao aliyokabidhiwa na
Mwenyekiti wa bodi wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi
URA-SACCOS, Naibu Kamishna wa Polisi, Thobias Andengenye. Ngao hiyo
alikabidhiwa jana kama ishara ya IGP kuwa balozi wa saccos hiyo katika
viwanja vya kilwa road wakati wa uzinduzi wa Tawi la URA-SACCOS la Kilwa
Road.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi, IGP Saidi Mwema akikata utepe kuashiria uzinduzi wa
tawi la Kilwa Road la Chama cha Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi
URA-Saccos jana jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Saidi Mwema akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa bahati nasibu ya kushindania pikipiki na cherehani
itakayochezeshwa na Chama cha Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi, Ura
Saccos tawi la kilwa road. Tawi hilo lilizinduliwa na IGP.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini , IGP Saidi Mwema akipasha na maofisa,
wakaguzi na askari wa Jeshi la Polisi, wakati wa uzinduzi wa Tawi la
Chama cha Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi Kilwa Road, Ura-Saccos
jana jijini Dar es Salaam.
Msemaji
wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Mwandamizi, Advera Senso akionyesha ngao
aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa bodi ya Chama cha Kuweka na Kukopa cha
Jeshi la Polisi, URA-SACCOSS. Ngao hiyo ni ishara ya kuwa balozi wa
SACCOS hiyo ambayo tawi lake la Kilwa Road lilizinduliwa jana na IGP. Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
………………..
Na Alex Mpeka, Jeshi la Polisi.
Askari
wametakiwa kutumia huduma zinazotolewa na Chama cha ushirika cha akiba
cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi (Ura- Saccos) ili
kujijiendeleza katika ujasiliamali pamoja na kuboresha maisha yao.
Hayo
yalisemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema jana wakati wa
mahadhimisho ya miaka saba (7) ya Ushirika huo, yaliyofanyika katika
viwanja vya Polisi Kurasini barabara ya Kilwa, jijini Dar es salaam.
Alisema
kuwa askari wanapopata mikopo katika ushirika huo wanakuwa hawana
wasiwasi wa kutozwa riba kubwa kwa kuwa ushirika huo lengo lake ni
kuinua ustawi wa askari na familia zao.
IGP
Mwema, alisema kuwa, Jeshi la Polisi hivi sasa linaendelea kutekeleza
program ya Maboresho, ambapo kupitia ushirika huo na kuweza kutoa jumla
ya shilingi billioni arobaini na mbili (42), ambazo zimetumika kwa ajili
ya kuboresha maisha ya askari na familia zao kwa lengo la kujiendeleza
kielimu, ujenzi wa nyumba ununuzi wa viwanja, kujikimu pamoja na
ujasiliamali.
Hata
hivyo, kwa upande wake Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi, Naibu
Kamishina wa Polisi (DCP), Thobias Andengenye, alisema kuwa, miongoni
mwa mafanikio yametokana na ushirikiano mzuri wa Benki ya CRDB ambapo
watendaji wa URA SACCOS wameweza kuendesha mafunzo na kuandaa semina
mbalimbali za kuwajengea uwezo na kufuata misingi ya sheria na taratibu
za sera ya vyama vya ushirika.
Aidha
katika maadhimisho hayo, IGP Mwema alizindua bahati nasibu ya weka
akiba na ushinde ambapo kupitia bahati nasibu hiyo wanachama wake
watapata fursa ya kushidania vyerehani kumi, pikipiki tano aina ya
boxer ambapo mshiriki atatakiwa kuwa na akiba ya isiyopungua laki tano
katika akaunti yake.
Pamoja
na mambo mengine IGP Mwema aliwakabidhi ngao mabalozi sita kutumia
nafasi walizo nazo kunadi URA SACCOS ambao ni Kamishina wa Polisi
Zanzibar (CP) Mussa Alli Mussa, Mkuu wa chuo cha Polisi moshi (MPA)
Kamishina msaidizi wa Polisi (ACP) Matanga Mbushi, Mkuu wa chuo cha
polisi dar es salaam, Ally Lugendo, Mkurugenzi wa Muziki wa Jeshi la
Polisi, Kamishina msaidizi (ACP) Haule, pamoja na msemaji wa Jeshi la
Polisi nchini Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Advera Senso
Chama
cha Ushirika cha kukopa cha Jeshi la Polisi (URA- SACCOS) Kilianza
mwaka 2006 na mpaka hivi sasa kimetimiza miaka saba ambapo kimeweza
kuboresha maisha ya askari na watumishi raia wanaofanya kazi Wizara ya
Mambo ya Ndani kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu ukilinganisha na benki
zingine za kibiashara.
No comments:
Post a Comment