Maelfu
ya waandamanaji wamejitokeza mwanzoni mwa wiki hii kupinga mashindano
ya Miss World yanayotarajia kuanza jumapili ya kesho nchini Indonesia
.Waandamanaji hao wametaka shindano hilo lifutwe kwani linadhalilisha
utu wa mwanamke na ni kinyume na mafundisho ya kiislamu.
Upinzani
mkubwa toka kwa waandamanaji hao umezidi, katika taifa hilo lenye
Waislamu wengi zaidi duniani,licha ya waandaaji kudai wameondosha vazi
la ufukweni (bikini)
Baadhi
ya wanaume na wanawake 800 kutoka kundi la Hizbut Tahrir la Indonesia
wamekusanyika katika mji wa Jakarta nje ya wizara ya ustawi wa jamii,
wakitoa wito kwa serikali wa kufuta shindano hilo.
Aidha
waliandamana hadi makao makuu ya shirika la habari la Indonesia MNC
kwamba liache kutangaza habari za shindano hilo lililopotoka. "Je,
tunataka nchi yetu kuonekana kama ya watu wa ngono?" mmoja wa waandamaji
alisema kwa sauti kubwa .
"Sisi
tutaendelea kuandamana na kuwaambia watu jinsi ya udhalilishaji
wanawake kwa kufanyika shindano hili," alisema mratibu wa maandamano
hayo, Zikra ASRI,huku akiwa amezungukwa na wanawake waliovaa hijabu
nyeupe na baibui nyeusi.
Baadhi ya Waandamanaji katika Picha. |
Mjini
Medani katika kisiwa cha Sumatra, wanachama 500 wa Hizbut Tahrir
waliandamana hadi majengo ya serikali, na kudai kuwa shindano hilo
lifutwe.Licha ya upinzani kuongezeka , waandaaji wamesema kuwa shindano
hilo lazima lifanyike na halita athiri heshima na utamaduni wa
indonesia
Shindano
la Miss Dunia linatarajiwa kuanza Jumapili katika kisiwa cha Bali, na
mshindi anatarajiwa kupatikana katika jiji la Jakarta Septemba 28.
Nchi
hiyo yenye watu milioni 240,June mwaka jana mwanamuziki Lady Gaga
alilazimika kufuta onesho lake,baada ya viongozi wa dini ya kiislamu
kutishia kuchoma moto ukumbi ambao atafanyia onesho hilo,baada ya
mwanamuziki huyo kuonesha mavazi yake ya ndani.
Kwa Habari zaidi tembelea HAPA
No comments:
Post a Comment