SHEIKH OMAR AL HAD OMAR |
Jamii ya Waislamu wamekumbushwa kwamba wana uwezo wa kuleta maendeleo katika jamii ya Kiislamu bila ya kuwategemea wafadhili.
Hayo yamesemwa jana na Imamu wa
Msikiti wa Kichangani Sheikh Omar Al had Omar alipokuwa anawahutubia Waislamu
waliofurika katika ibada ya Swala ya jumaa.
Amesema iwapo tutatambua na
kuthamini kwamba sisi binaadamu tuna dhamana ya uongozi katika dunia hii,tunaweza
kabisa licha ya unyonge wetu huu tukaleta mabadiliko makubwa yenye tija kwa
waislamu na jamii kwa ujumla.
“Nakubali kabisa kwamba
tatizo kubwa ni kwa baadhi ya viongozi kutokuwa na muono wa mbali na wengine
kukosa uaminifu,lakini sina shaka na waislamu kwamba wanataka maendeleo ya kweli,sasa
hawa waislamu wanaotaka maendeleo ya kweli wakionyeshwa njia yenye usimamizi
madhubuti tunaweza kabisa kupata maendeleo bila kutegemea wafadhili”.
"Ndugu zangu Waislamu,leo sisi
tumekuwa wahanga wa maendeleo karne kwa karne,Serikali inapotoa huduma
haiangalii imani ya watu,bali inatoa huduma kwa kuangalia umuhimu wa
huduma,kutokana na hali hiyo sisi tumekuwa na wahanga wa huduma hizo katika
sekta mbalimbali,ikiwemo sekta ya afya,na katika sekta hii muathirika mkubwa ni
mwanamke wa Kiislamu,leo akitaka kupata huduma ya Utra Sound ni lazima avua
nguo na haijalishi anayempatia huduma hii ni mtu wa jinsia gani,hatimaye
mwanamke huyu anaipokea huduma hii kwa udhalili mkubwa na kwa unyonge mkubwa,lakini
haya yanawezekana kwetu tukaondokana nayo kama tukiwa na mipango madhubuti
yenye usimamizi imara”.
Akiongea kwa hisia Sheikh Omar
aliendelea kusema”sisi waumini wa
masikti wa kichangani tumeliona hilo na tumeamua kwa kila Swala waumini
kuchanga shilingi mia mbili ambazo tayari zimeshaanza kuonesha matunda
makubwa,tunatoa wito kwenu ndugu zetu mutuunge mkono kwani huu ndiyo wakati wa
mabadiliko,tusisubiri mjomba aje kutusaidia”,.
Kufuatia hamasa hiyo munirablog usiku ilimfuata Sheikh Omar
nyumbani kwake mtaa wa Uwazani na kufanya mahojiano ya kina na kugundua kwamba
anashehena ya mipango ya maendeleo ambayo kama
atapata watu wenye ikhlaswi na moyo wa kujitumia jamii ya kiislamu inaweza
kutoka katika mnyororo wa fikra tegemezi.
Wakati huo huo blog,katika
hali ya kuunga mkono harakati hizo munirablog itakuwa inatoa takwimu za mapato
kwa kila alkhamis sambamba na kufuatilia mchakato mzima wa harakati hizo kwa
manufaa ya waislamu
UFUATAO NI MCHNGANUO MFUPI WA
MAPATO.
TAREHE
|
ADHUHUR
|
SWALA YA IJUMAA
|
AL ASRI
|
MAGHRIB
|
ISHAA
|
JUMLA
|
|
1
|
2/9/13
|
53,000/
|
101,000
|
46,000/
|
50,000
|
250,000
|
|
2
|
3/9/13
|
93,000
|
44,000
|
61,000/
|
52,300
|
250,300/
|
|
3
|
4/9/13
|
58,000/
|
82,000/
|
140,000/
|
|||
4
|
5/9/13
|
85,000/
|
42,000/
|
86,000/
|
50,000/
|
263,000/
|
|
5
|
6/9/13
|
1,000,000/
|
1,000,000/
|
No comments:
Post a Comment