Sunday, September 08, 2013

KUTOKA MUNIRA MADRASA BLOG : WAISLAMU TUSHIRIKIANE KULETA MAENDELEO



MZEE HAROUB DAWA MWITA.

Wito umetolewa kwa Waislamu wa ndani na nje ya nchi kushirikiana na Taasisi ya Munira Madrasa And Islamic Propagation Association ili kuleta maendeleo yanayokusudiwa kwa faida ya jamii kwa ujumla.

Hayo yamesemwa jioni hii na Mshauri Mkuu wa Miradi na Uchumi wa Taasisi hiyo Mzee Haroub Dawa Mwita alipotambulishwa rasmi rasilimali zinazomilikiwa na Taasisi hiyo.

"Nimefurahi sana kunileta hapa (mlandizi) na kunionyesha rasilimali hii (ardhi) yenye ukubwa wa heka kumi,kwa hakika mumefanya juhudi kubwa sana kulipata eneo hili,sasa kazi iliyopo mbele yetu ni kuhakikisha tunapiga hatua zaidi,lakini sisi munira peke yetu hatuwezi kufanikisha haya bila ya wenye uwezo wa ndani na wa nje ya nchi kushirikiana nasi,naamini tukishirikiana kwa pamoja tutafikia maendeleo kwa uwezo wa ALLAAH".mwisho wa kumnukuu.

Aidha alisema atajitahidi kutumia taaluma yake kuishauri taasisi ya munira kwa kadri atakavyoweza ili ifikie malengo yake.

kitaaluma mzee Haruob Mwita ni Mhasibu na ana Diploma ya Uhasibu aliyoipata mwaka 1980 katika chuo cha Mzumbe,aidha amefanya kazi ya Uhasibu na Ukaguzi wa mahesabu kwa zaidi ya miaka ishirini.
Taasisi ya Muniira Madrasa ambayo ni wamiliki wa blog hii,ina Ardhi yenye ukubwa wa heka kumi na wanakusudia kujenga Shule ya Sekondari (intergred). mbali ya hayo kwa mujibu wa ramani yao kutakuwa na zahanati,msikiti,madrasa ya kisasa na nyumba za waalimu.
Ardhi hiyo ipo Mlandizi Mkoa wa Pwani,Kilomita nne kutoka Barabarani (msufini stend).

PICHA ZA ENEO LA ARDHI INAYOMILIKIWA NA MUNIRA.



MUANGALIZI WA KIWANJA AKIMUONESHA MIPAKA MZEE HAROUB NA VIONGOZI WAANDAMIZI WA TAASISI YA MUNIRA.

KATIBU MKUU WA TAASISI YA MUNIRA MADRASA UST JUMA RASHID AKIANDAA MAZINGIRA YA KUWEKA ALAMA KATIKA MIPAKA YA ENEO WANALOLIMILIKI.
 

HADI KULEEE,NDIVYO ANAVYOONEKANA KUSEMA MUANGALIZI WA KIWANJA HICHO MBELE YA VIONGOZI WA TAASISI YA MUNIRA,KUSHOTO NI UST OMAR SAID SALUM CHONDOMA,AMBAYE NI MWEKA HAZINA WA TAASISI YA MUNIRA.

MZEE HARUOB AKISAFISHA ENEO TAYARI KWA KUWEKA ALAMA KATIKA MIPAKA HIYO.

MWANGALIZI WA KIWANJA AKISHUSHA CEMENT NA KOKOTO KWA AJILI YA KUIMARISHA MIPAKA YA KIWANJA HICHO.

KATIBU MKUU UST JUMA RASHID NA MSHAURI MKUU WA MIRADI NA UCHUMI MZEE HAARUOB WAKIFURAHIA MAELEKEZO KUTOKA KWA MUANGALIZI WA KIWANJA HICHO KILICHOKO MLANDIZI MKOA WA PWANI.

BAADA YA KAZI,WATENDAJI WA TAASISI YA MUNIRA WALIINGIA MSIKITINI KWA AJILI YA SWALA YA AL ASWIR. 
PICHA NA HABARI KUTOKA MUNIRAMADRASA BLOG .

1 comment:

  1. Anonymous1:09 PM

    Hongereni Taasisi ya Munira Madrasa And Islamic Propagation Association

    ReplyDelete