NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
WAZIRI
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi amewataka waganga wa
tiba asili washirikiane na wataalamu wa utafiti ili kuwezesha
upatikanaji wa dawa bora na salama.
Kauli
hiyo ilitolewa leo na Waziri huyo wakati akitoa tamko kuhusu
maadhimisho ya siku ya tiba ya asili ya mwafrika ambayo huadhimishwa
kila mwaka Agosti 31, lakini mwaka huu hayakufanyika kutokana na uhaba
wa fedha. Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika mwakani kipindi
katika hicho.
“
Tanzania tunayo mitidawa mingi na mingi haijafanyiwa kazi katika utafit
na kuweza kubaini uwezo wa kutibu magonjwa mbailmbali tatizo lililopo
ni jinsi gani mitidawa hiyo inweza kufanyiwa utafiti na kuwa dawa bora
na salama kwa watumiaji kwa kuziwekea mifumo ya huduma za afya ili kila
mwenye kuhitaji aweze kuzipata,” alisema Dk. Mwinyi .
Dk.
Mwinyi aliwataka waganga hao kushirikiana na watafiti kutoka Taasisi ya
Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Taasisi ya
Utafiti wa Dawa za Asili iliyokpo katika Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi Shiriki- (MUHAS).
Aliongeza
kuwa waganga wote wa tiba asili na tiba ya kisasa wanatakiwa kufanya
kazi kwa kuelewana ili kuwezesha kupata taarifa za awali kabla ya
utafiti kamili kufanyika.
Aliitaja
kauli mbiu ya maadhimisho hayo kuwa ni ‘ Tiba Asili : Utafiti na
Maendeleo’ kuwa inalenga kutoa majukumu kwa waganaga wa tiba asili na
tiba mbadala katika sula zima la utafiti. Pili inatoa changamoto juu ya
uendelezaji wa taarifa za utafiti wa mitidawa katika kutafuta dawa ya
kutibu magonjwa mbalimbali.
Aidha aliwahimiza waganga wa tiba asili kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao na huduma za afya.
No comments:
Post a Comment