NA ELIPHACE MARWA – MAELEZO
MAKAMU
wa Rais Dkt. Mohamed Ghalib Bilal ameutaka Wakala wa Majengo
Tanzania(TBA) kuangalia jinsi ya kutumia fursa amabayo Serikali
imeruhusu taasisi za Serikali kuingia ubia ba sekta binafsi(PPP)katika
kufanikisha miradi ya ujunzi wa nyumba za watumishi wa umma.
Kauli
hiyo ilitolewa leo na Makamu wa Rais wakati sherehe za uweka ji wa
jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba 851 za watumishi wa umma katika eneo
la Bunju B, wilaya ya kinondoni Jijini Dar es Salaam.
“
Wakala mnatakiwa muangalie jinsi ya mtakavyoweza kutumia wabia wa
ndani na wa nje katika kutekeleza mradi maalum wa ujenzi wa nyumba
10,000 kwa kipindi cha miaka mitano ambao unatazamiwa kutatua kero ya
makazi ya watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla,” alisema Dkt. Bilal.
Makamu
wa Rais aliongeza kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kazi bora
inayofanywa na watumishi wake ndiyo maana inawaonesha kuwajali kwa
kuwajengea nyumba bora .
Aidha
aliupongeza wakala huo, kwa kuanzisha mradi huo wa kujenga nyumba
hizo,ambapo gharama ya nchini inaanzia milioni 25 hadi kufikia milioni
50.
Naye
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akielezea changamoto mbalimbali
ambazo wakala huo, unaakabiliana nazo kuwa ni gharama kubwa za
uwekaji miundombinu ya maji safi na nishati.
Alizitaja
changamoto nyingine ni kutozwa riba kubwa za mikopo zinazotolewa na
benki za hapa nchini, pia baadhi ya halimashauri kutokuwa na viwanja
vya kutosha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.
“
Naomba Makamu wa Rais na ofisi yako inisaidie kuhakikisha wale wote
ambao wanadaiwa mikopo ya nyumba wawe wamelipa ndani ya mwezi mmoja
ikiwa watashindwa kulipa wanyang’anywe nyumba hizo na kuuziwa watu
wengine ili kutoa fursa kwa wakala kujenga nyumba nyingine , ambapo hadi
sasa watu 2500 bado hawajamaliza kulipa madeni yao,” alisema Waziri
Magufuli.
Aidha
wakala huo, utajenga nyumba nyingine 1400 katika mkoa wa Dares
Salaam na nyumba 2500 katika mikoa 12 ya Tanzania Bara kwa kipindi cha
mwaka huu wa fedha wa 2013/2014 na kumalizia nyumba zilizo baki ndani
ya miaka mitatu, ambapo Makamu wa Rais alitaka ujenzi huo usisimame ili
kufikia lengo la nyumba 10,000 na zaidi.
No comments:
Post a Comment