Sunday, October 27, 2013

MAHAFALI YA KWANZA YA SHULE YA WAMA NAKAYAMA YATIKISA NYAMISATI RUFIJI‏


 

Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wageni waalikwa na wahitimu wakati wa mahafali hayo jana huko Nyamisati Rufiji.

2

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Shule ya WAMA Nakayama Suma Mensa na viongozi mbalimbali.…

Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wageni waalikwa na wahitimu wakati wa mahafali hayo jana huko Nyamisati Rufiji.

2

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Shule ya WAMA Nakayama Suma Mensa na viongozi mbalimbali.

4

Watu mashuhuri na viongozi mbalimbali wakiwa katika mahafali hayo.

5

Mama Salma Kikwete akiwasili katika eneo la tukio kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa shule hiyo Dk. Ramadhan Dau.

1
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama Salma Kikwete Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo WAMA wakati alipowasili katika viwanja vya mahafali katika mahafali ya Kwanza ya Shule ya Sekondari WAMA Nakayama yaliyofanyika katika shule hiyo iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani jana. Zaidi ya wanafunzi 60 walitunukiwa vyeti vya kumaliza kidato cha nne na zawadi mbalimbali zilitolewa kwa wahitimu wakati wa mahafali hayo ambayo yalihudhuriwa pia na viongozi na watu mashuhuri akiwemo balozi wa Japan na wafanyabiashara ambapo mwenyekiti wa IPP, Dk. Reginald Mengi aliahidi kuisadia shule hiyo shilingi milioni 200 kila mwaka kwa miaka mitano ambazo ni kiasi cha shilingi bilioni moja kwa miaka hiyo mitano.
5a

Wahitimu wakiingia katika eneo la tukio.

6

Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akicheza na wanawake wenzake ambao ni wake wa viongozi.

6b

Rais Jakaya Kikwete wa nne kutoka kulia akiwa na viongozi mbalimbali katika meza kuu wakiimba wimbo wa taifa ulioongozwa na wanafunzi wa shule ya WAMA Nakayama kutoka kulia ni Balozi Tanzania, Mhe. Masaki Okada Mkuu wa Mkoa wa Pwani Ndugu Mwantumu Mahiza, Mama Salma Kikwete na kutoka kushoto ni Dk. Ramadhan Dau Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Wama Nakayama na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa.

 7

Baadhi wa walimu wa shule hiyo.
7c

Baadhi ya wanakamati kutoka kulia ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage, Daudi Nasibu Katibu Mkuu Taasisi ya WAMA na Dan Kiondo.
8

Baadhi ya wananfunzi wa shule ya WAMA Nakayama.
8c

Mbunge Vick Kamata akiongoza wanafunzi wa Wama Nakayama kuimba wimbo maalum kwa wahitimu katika mahafali hayo.
9

Viongozi mbalimbali wakicheza muziki wakati wa mahafali hayo.
9d

Dk. Ramadhan Dau Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Wama Nakayama akizungumza katika mahafali hayo.
10

Mama Salma Kikwete akikaribisha wageni mbalimbali katika mahafali hayo.
10e

Mkuu wa Shule ya WAMA Nakayama, Suma Mensa akitoa historia ya shule hiyo.
10g

Mmoja wa wasanii wa kundi la Mjomba Band linaloongozwa na msanii Mrisho Mpoto akiigiza katika igizo maalum lililokuwa likitafsiri changamoto zinazomkabili mtoto wa kike yatima na anayeishi kwenye mazingira magumu katika suala zima la kupata elimu.
11

Mkuu wa Wilaya ya Kionondoni Ndugu Jordan Lugimbana pamoja na waalikwa wengine katikati akiwa katika hafla hiyo.
11h

Wahitimu wakiimba wimbo maalum wa kumshukuru Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete.
13

Nyoka alikuwa ni moja ya burudani katika mahafali hayo.
18

Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Regnald Mengi akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza. Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Aisha Bilal.
19

Baadhi ya majengo ya shule hiyo.
20 21

Mdau Seraphin kutoka Serena Hotel alihudhuria pia.
22

Mama Salma Kikwete katikati akiimbiwa wimbo maalum na wahitimu.
23

Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakicheza wimbo maalum ulioimbwa na wanafunzi wahitimu katika mahafali hayo.
24

Rais Jakaya Kikwete na Mkewe mama Salma Kikwete wakiongoza viongozi mbalimbali kucheza wimbo huo.
26

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na makundi mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa mahafali hayo jana.
 27 28 29 
PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-NYAMISATI RUFIJI.

No comments:

Post a Comment