Rais
Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiangalia majani ya chai
yaliyofikishwa katika kiwanda cha chai cha Ikanga kwa ajili ya
kusindikwa. Kiwanda hicho kilizinduliwa rasmi na Rais Kikwete tarehe
18.10.2013.
Rais
Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiangalia chai iliyosindikwa na
kufikia hatua ya mwisho kabla ya kufungwa kwenye pakiti huku wakipata
maelezo kutoka kwa Meneja Msaidizi wa Kiwanda cha chai cha Ikanga Bwana
Flowin Msigwa .
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimia mamia ya wananchi wa kijiji cha
Wanginyi kilichoko katika kata ya Lupembe, wilayani Njombe kwa
kuwapungia mikono mara baada ya Mama Salma na Rais Kikwete kuwasiri
kijijini hapo kwa ajili ya mkutano wa hadhara tarehe 18.10.2013
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia bidhaa mbalimbali
zinazotengenezwa na akinamama wa kikundi cha Jitegemee wakati wa
maonyesho yaliyofanyika mjono Njombe kwa ajili ya sherehe za uzinduzi
rasmi wa mkoa wa Njombe huku kiongozi wa kikundi hicho Mama Leokadia
Kaduma akimfafanulia juu ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na
wanakikundi ha
Chipukizi
wa Mkoa wa Njombe wakicheza halaiki wakati wa sherehe ya ufinguzi
rasmi wa Mkoa wa Njombe zilizofanyika tarehe 18.10.2013.
Rais
Jakaya Kikwete akibonyeza king’ora huku wazee wawili wa kimila wakiwa
wamewashika njiwa na baadare kuwarusha hewani kuashiria kuzinduliwa
rasmi kwa mkoa wa Njombe katika sherehe zilizofanyika mjini Njombe
tarehe 18.10.2013.
Rais
Jakaya Kikwete akiambatana na Mkewe Mama Salma Kikwete wakipokea
taarifa fupi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mufindi Tea Company Group
Bwana Noel Smith, kuhusu kukamilika kwa kiwanda cha chai
walichokijenga katika kijiji cha Ikanga kilichoko katika Kata ya
Lupembe, wilayani Njombe ambacho Rais Kikwete alikizindua rasmi tarehe
18.10.2013.
PICHA NA JOHN LUKUWI
No comments:
Post a Comment