PICHA ZA SWALA NA BARAZA LA IDD EL HAJJ ZANZIBAR
Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wapili kushoto akiwapamoja na viongozi na
wananchi mbalimbali katika Swala ya Idi –El-Hjji ilioswaliwa Kitaifa
huko katika kitongoji cha Marumbi Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja.
Wananchi waliohudhuria katika Baraza la Idi-El-Hajji lililofanyika huko Tunguu Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja
Baadhi
ya Viongozi na Wananchi waliohudhuria katika Baraza la Idd -El-Hajj
lililofanyika huko Tunguu Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja
Waumini wanawake katika swala ya Idd
Kinamama katika baraza la Iddi
Rais
wa Zanzibar Dkt Mohamed Ali Shein akiwa pamoja na Makamo wa Kwanza wa
Rais Maalim Seif Sharif Hamad mara baada ya kumalizika kwa Baraza la la
Idi -El-Hajji lililofanyika huko Tunguu Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati
Unguja
Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akisalimia wananchi baada ya wala ya Idd
–El-Hajj ilioswaliwa Kitaifa huko katika kitongoji cha Marumbi Mkoa wa
Kusini Wilaya ya Kati Unguja.
Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akitoa hotuba katika baraza la Idd
-El-Hajj lililofanyika huko Tunguu Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja
Baadhi
ya Viongozi na Wananchi waliohudhuria katika Baraza la Idi-El-Hajji
lililofanyika huko Tunguu Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja
Sehemu ya kinamama katika baraza la Idd
Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akitoa hotuba katika baraza la Idi
-El-Hajji lililofanyika huko Tunguu Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja
Dua katika Baraza la Idd
Na
Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 16/01/2013
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
ameendelea kusisitiza hali ya Amani na kukemea Vitendo vinavyofanywa na baadhi
ya Watu wachache wenye lengo la kuiharibu sifa ya Zanzibar.
Amesema
tangu Karne zilizopita Zanzibar pamekuwa pahala pa Amani na utulivu na hivyo
kuitaka jamii kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa vyombo vya ulinzi na usalama
ili kuwafichua watu ambao wanaoharibu Amani iliyopo.
Rais
Shein ameyasema hayo leo katika Hotuba yake aliyoitoa katika Baraza la Idd
lililofanyika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema
kiujumla hali ya Amani na Utulivu imetanda kote katika Visiwa vya Zanzibar hali
inayopelekea Serikali kupanga na kutekeleza mipango yake ya kimaendeleo kwa
lengo la kuimarisha uchumi na ustawi wa Wananchi wake.
Hata
hivyo amekea tabia inayofanywa na baadhi ya Watu wachache wanaowahujumu na
kuwatia hofu Wananchi pamoja na Wageni wanaoitembelea Zanzibar.
Amefahamisha
kuwa hakuna Dini inayowaelekeza waumini wake kuwahujumu Wanadamu wengine na
kwamba watakaobainika kufanya vitendo hivyo watachukuliwa hatua kali za
kisheria.
Amewahahakikishia
Wananchi na Wageni kwamba vyombo vya Ulinzi na usalama vinafanya kazi nzuri ya
kusimamia ulinzi na Usalama na kuitaka jamii kutoa ushirikiano unaohitajika.
Aidha
Dkt. Shein amebainisha kuwa kutokana na kuimarika kwa hali ya usalama na amani
Uchumi wa Zanzibar unaendelea kukua kwa kiwango cha kuridhisha kutoka Asilimia
6.7 kwa mwaka 2011 hadi Asilimia 7.0 mwaka 2012.
Ameongeza
kuwa hali hiyo inatoa matumaini makubwa hasa ikizingatiwa kuwa ukuaji wa uchumi
katika Bara la Afrika ni Asilimia 5.3
ambapo kwa upande wa Ukuaji wa uchumi wa Dunia ni Asilimia 2.9
Kuhusu
Zao la Karafuu Dkt. Shein amesema kuwa Shirika la Biashara la Taifa ZSTC
linatarajia kununua tani 4,016 kwa mwaka 2013 na kuwaomba Wananchi waendelee
kushirikiana na Serikali katika kupambana na watu wanaofanya Magendo ya
Karafuu.
Awali
Akimkaribisha Rais Shein kutoa Hotuba yake Waziri wa Katiba na Sheria Aboubakar
Khamis Bakary alisema Serikali imepanga Sala na Baraza la Idd katika Siku kuu
zote za IDD-EL HAJJ zitakuwa zikifanywa kitaifa katika Mikoa yote ya Unguja na
Pemba ambapo kwa mara hii Swala ya Idd ilifanyika kijiji cha Marumbi Mkoa wa
Kusini Unguja.
alifahamisha
kuwa Serikali imeamua kufanya hivyo ili Wananchi wa Mikoa yote ya Unguja na
Pemba wapate fursa ya kuswali pamoja na Viongozi wao Wakuu wa Kiserikali lakini
kwa upande wa Swala ya IDD EL-FITRI itaendelea kuswaliwa kitaifa katika Mkoa wa
Mjini Magharibi.
Sherehe
ya IDD EL HAJJ inakuja kila mwaka kufuatia kumalizika kwa Ibada ya Hijja
inayofanyika MAKKA Nchini Saudia kwa Waislamu wenye uwezo wa kufanya Ibada
hiyo.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 16/01/2013
No comments:
Post a Comment