JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI,VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Idara
ya Habari – MAELEZO, inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kwamba
Mheshiwa Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo amepokea maombi kutoka kwa wamiliki wa Magazeti ya Mwananchi na
Mtanzania wakiomba kupunguziwa adhabu au kusamehewa adhabu
wanazozitumikia kuanzia 27 Septemba, 2013.
Wakati
Mheshiwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo anatafakari
maombi hayo, amesikitishwa kuona kwamba magazeti haya mawili yamekiuka
masharti ya adhabu walizopewa .
Wamiliki
wa Gazeti la Mtanzania baada ya kufungiwa wameamua kuligeuza gazeti la
kila wiki la RAI kuwa la kila siku bila ya kibali cha Msajili wa
Magazeti. Kwa mujibu wa ratiba ,gazeti la RAI linapaswa kutoka kila
siku ya Alhamisi .
Wamiliki wa gazeti la Mwananchi nao wameendelea kuchapisha gazeti hilo katika mtandao kinyume na agizo la kufungiwa.
Serikali
inawataka wamiliki wa vyombo habari nchini kuwa na utamaduni wa kutii
sheria za vyombo vya habari zinazotumika wakati huu. Hivyo serikali kwa
mara nyingine tena inawataka wamiliki wa Gazeti la MTANZANIA,
kuzingatia ratiba yao ya kutoa gazeti lao kila siku ya ALHAMISI,
Aidha,
serikali inawataka wamiliki wa Gazeti la Mwananchi kuacha mara moja
kuchapisha gazeti lao katika mtandao kama amri ya kufungiwa
ilivyoanisha.
Imetolewa na,
Idara ya Habari – MAELEZO
10 Oktoba, 2013
No comments:
Post a Comment