Kutoka
kushoto ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dkt. Philip
Mpango, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Silvacius Likwelile, Kamishna
wa Sera Bw. Beda Shallanda na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Said Magonya
wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa majadiliano ya mkutano wa
madola. Picha zote na Bi. Eva Valerian – Washington DC
Mwenyekiti wa majadiliano ya mkutano wa Madola Bw. Sheku Sesay akifafanua jambo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia majadiliano; mwenye tai nyekundu ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Silvacius Likwelile.
…………………………………………………………………………………..
Wakati
mikutano mingine ikiendelea hapa mjini Washington DC, Tanzania pia
inashiriki katika mkutano wa Jumuiya ya Madola ambao utafanyika kwa siku
mbili mfululizo. Mkutano huu unahudhuriwa na wajumbe wote ambao ni nchi
wanachama.
Katika
mkutano huo kikubwa kilichojadiliwa ni kuhusiana na suala zima la
biashara, ni namna gani biashara inaweza kufanyika na kwamba nchi zetu
haziko vizuri sana katika uwanja huu wa kimataifa. Katika mkutano huo
walijadili ni jinsi gani wanaweza kufanikisha lengo la kuanzisha mfuko
ambao utatumika kusaidia biashara ‘trade facilitation’.
Katika
majadiliano yaliyokuwa yakifanyika wajumbe wengi walipenda kujua kwamba
ni tofauti gani mfuko huo mpya utaleta ili nchi zetu ziweze kunufaika.
Hiki ni kitu kikubwa zaidi kilicho wagusa wajumbe wengi.
Akizungumza
na vyombo vya habari Dkt. Silvacius Likwelile ambaye ni Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha ambaye alisema kuwa”katika mkutano huu jambo ambalo
limezungumziwa sana ni kuhusu kuondoa vikwazo ambavyo mara nyingi
tunawekewa ili kufikia masoko katika ulimwengu”.
Aliendelea
kusema kuwa, ni imani yetu kwamba tume ya madola itafanyia kazi masuala
hayo ili hatimaye tuwe na msimamo mmoja wa kuweza kusaidia ukuaji wa
biashara katika nchi zetu.
Mkutano huu utaendelea tena kesho na inategemewa utakuwa na mafanikio makubwa.
Imetolewa na:
Ingiahedi Mduma
Msemaji Mkuu
Wizara ya Fedha
Washington D.C
No comments:
Post a Comment