Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Advocatus Kakorozya akimwelezea
jinsi tasisi inavyotumia teknologia kupata taarifa mbalimbali za afya
ambazo zimesaidia sana serikali kutunga sera.
Rais
Jakaya Kikwete jana (Jumatano) alitembelea kituo cha Bagamoyo ya
Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) na kuonyeshwa kazi mbalimbali za
utafiti zinazofanyika kituoni hapo. Raisi Kikwete aliisifia taasisi hiyo
kwa kufanya kazi kubwa hasa katika upande wa ugonjwa wa Malaria na
kujipatia sifa kubwa duniani.
Rais
Kikwete akimsikiliza mtafiti wa IHI Dk Nico Govella akimpa maelezo juu
ya utafiti wake ambapo magunia ya katani yakichanganywa na kemikali
fulani yanaweza kutumika kukinga wanadamu dhidi ya mbu wanaoeneza
malaria.
Rais Kikwete akimsikiliza Grace Mwangoka wa IHI akimweleza shughuli mbalimbali za maabara kwenye taasisi hiyo.
Rais
Kikwete akimsikiliza Joseph Madata ambaye ni mkutubi akimwelezea
matumizi ya maktaba mtandao (digital library) ya taasisi hiyo.
Rais
Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa IHI pamoja na
wenzao kutoka Equatorial Guinea ambao wapo kwenye kituo hicho cha
Bagamoyo kwa ajili ya mafunzo.
No comments:
Post a Comment