Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoka kuweka jiwe la msingi madarasa ya kidato cha tano shule ya sekondari lupalilo.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiongea na Bi
Sarah Mageni Sanga, mlemavu ambaye Rais alimpa pikipiki ya Bajaji pamoja
na mtaji wa pesa taslimu wa shilingi milioni mbili October 28, 2009
baada ya kuguswa na mkasa wa maisha ya mkaazi huyo wa kijiji cha
Lupalilo wilaya ya Makete mkoa wa Njombe alipomuona akohojiwa katika TV
na kueleza kuwa maisha yake ni magumu.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wananchi wa kijiji cha Ivalalila
wilayani Makete baada ya kuweka jiwe la msingi la kituo cha afya cha
kijiji hicho mwishoni mwa juma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA cha Wilaya ya Makete mwishoni mwa juma.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia ubora wa shati lililotengenezwa na
wanafunzio wa Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA cha Wilaya ya Makete baada
ya kukifungua rasmi chuo hicho mwishoni mwa juma.
No comments:
Post a Comment