Kundi la Wanafunzi Ishirini wa Kituo cha Kiislamu cha Kimisri kilichopo Chang'ombe Dar es salaam wanaondoka leo usiku kuelekea nchini Misri.
Wanafunzi hao wanakwenda nchini misri kujiunga na chuo Kikuu cha Kiislamu (Azhar Sharif) nchini humo.
"Wanaondoka leo majira ya saa saba usiku kwa ndege ya Egypt Air"alisema Ustaadh Said Zubeir ambaye ni mwalimu mwandamizi wa kituo hicho alipozungumza na Munira blog jioni hii.
Amesema wanatarajiwa kuanza masomo mara baada ya kufika na watasoma kwa miaka saba.
Wanafunzi hao jana walifanyiwa hafla fupi ya kuagwa,hafla ambayo iliongozwa na mudiir wa kituo hicho Dr Osama mahamoud.
Azhar Sharif ni moja katika vyuo vikubwa vinavyoheshimika duniani na vimetoa wanazuoni wengi sana.
USTAADH
MUHAMAD KHAMIS MMOJA YA WANAFUNZI WANAOSAFIRI LEO USIKU AKIFANYA
MAHOJIANO NA MWANDISHI WA HABARI NJE YA CHUO CHA KIISLAM CHA
KIMISRI,KILICHOPO CHANG'OMBE.
SHEIKH YAHYA MKALI AKITOA MAELEZO MACHACHE KWA WASAFIRI HAO.
WANAFUNZI WAKIWA NJE YA CHUO.
Habari na Picha kwa Hisani ya Munira Blog .
No comments:
Post a Comment