Monday, June 04, 2012

AINA ZA MAJI KWA KUZINGATIA SIFA ZAKE


Asalam alaykum Warahmatu Allahi Wabarakatu. 
Ndugu yangu katika Imani Baada ya Kuona Aina za Maji ambayo yanafaa kutumika kwa Ajili ya Twahara leo kwa Uwezo wake ALLAH tuyaangalie hayo Maji kwa kuzingatia sifa na hukumu zake.
kwa kuzingatia kigezo ambacho tumetangulia kukisema Maji yanagawanyika katika sehemu/mafungu matatu

1: MAJI TWAHUUR(MASAFI) au MAJI MUTLAQ
Maji haya yana sifa kuu mbili

1.Yenyewe ni twahara.
2.Yana uwezo wa kutwaharisha.
Maji yenye sifa hizi ni kama vile maji ya :-
1.mvua,
2.bahari,
3.maziwa,
4.mito,
5.chemchem
6.visima.

Maji haya yatafaa kutumika katika twahara muda wa kubakia katika jumbile lake la asili bila ya kubadilika mojawapo ya sifa zake tatu ambazo ni:-

1.rangi
2.Tamu (ladha)
3.Harufu (riha)

HUKUMU:

Hukumu ya maji haya ni kwamba yanaondosha hadathi zote mbili kubwa na ndogo, na najisi. Maji haya pia hutumika kwa kunywa, kufulia, kupikia, na shughuli nyingine za maisha ya kila siku ya mwanadamu.
2: MAJI TWAHARA:
Haya ni maji ambayo yana sifa moja tu ya kuwa yenyewe ni twahara lakini hayana uwezo wa kutwaharisha.
Maji haya yamechanganyika na kitu ambacho ni twahara kama vile sabuni, sukari, zafarani, unga, asali au maziwa na kitu hiki kikaharibu moja wapo ya sifa zile tatu za maji yaani :-
1.rangi,
2.ladha,
3.harufu.
Kuharibika huku kwa mojawapo ya sifa za maji ndiko kunakoyanyang’anya maji vile uwezo na nguvu yake ya kutwaharisha.

HUKUMU YAKE.
Hukumu ya maji haya yenyewe ni twahara na yanaweza kutumika katika matumizi mengine yote ya mwanadamu kama vile kunywa, kuoshea vyombo N.k ila hayawezi kutumiwa katika suala zima la twahara kama vile kuondosha hadathi ndogo (kutawadha),hadathi kubwa (kukoga) na kuondosha najisi.

3: MAJI NAJISI
Haya ni maji yaliyonajisika kwa kuingia ndani yake najisi itakayoharibu mojawapo ya zile sifa tatu za maji.
HUKUMU YAKE.

Hukumu ya maji haya ni kutokufaa kutumika katika twahara na matumizi mengine ya kila siku ya mwanadamu.
Mpaka hapa Nina Imani Ndugu yangu Kijana Mwenzangu tutakuwa tunaenda sawa katika Ukumbusho wetu unao husiana na Twahara Inshallah Ukumbusho ujao utahusu
au Tutaangalia Mgawanyo wa Maji kwa Kuzingatia wingi wake na Uchache wake.
UMOJA MSHIKAMANO NDIO KAULI MBIU YETU KWA PAMOJA DAIMA TUNAWEZA EWE M/MUNGU TUSAIDIE KUTUPA UWEZO WA KUFANYA MAMBO YA KHERI

No comments:

Post a Comment