Monday, June 04, 2012

MGAWANYIKO WA MAJI KWA KUZINGATIA WINGI NA UCHACHE


Ndugu zangu katika Imani kwa kukumbushia tayari tumeshaona Nini Maana ya Twahara,Vitu ambavyo tunavitumia kwa Ajili ya kujitwaharishia Baada ya hapo tukazungumzia aina za Maji ambayo waweza kuyatumia kwa ajili ya Twahara kisha tukazungumzia Mgawanyo wa Maji na Hukumu zake leo Inshallah Tunamaliza kwa kuangalia 

MGAWANYIKO WA MAJI KWA KUZINGATIA WINGI NA UCHACHE
Tukiyaangalia maji kwa kuuzingatia wingi na uchache wake tutayakuta yamegawanyika sehemu/mafungu mawili:-

1.maji mengi
2.Maji machache

MAJI MENGI
Haya kwa mtazamo wa sharia ni yale yaliyofikia kullatein na zaidi yake.
Kullatein ni miongoni mwa vipimo vilivyokuwa vikitumiwa na Waarabu zamani. Kwa vipimo tuvitumiavyo leo kullatein ni sawa na lita 216 za ujazo. Kwa vipimo vya ukubwa Kullatein ni sawa na dhiraa moja na robo upana, urefu na kina. Dhiraa moja ni sawa sawa na sentimeta 48 (48 cm)

HUKUMU YA MAJI MENGI
Maji yaliyofikia kullatein na kuendelea hayanajisiki kwa kuingia tu najisi ndani yake bali ya kuwa yamenajisika ikiwa najisi hiyo itaharibu mojawapo ya zile sifa tatu za
maji ambazo ni
1.rangi
2.Tamu (ladha)
3.Harufu (riha)

MAJI MACHACHE
Maji yatahukumiwa kuwa ni machache ikiwa hayakufikia kiwango cha kullatein yaani yako chini ya lita 216 za ujazo ambazo ni karibu ya madebe 12 yaliyojaa.

HUKUMU YA MAJI MACHACHE
Maji haya yatanajisika kwa kuingiwa na najisi hata kama najisi hiyo haikuharibu
mojawapo ya sifa za maji, na yatahukumiwa kwa mujibu wa sheria kuwa ni maji najisi na tayari tumekwisha itaja hukumu ya maji najisi huko nyuma.
Mpaka hapa Inshallah Tutakuwa tumemaliza Ukumbusho wetu wa Twahara Mungu akipenda tutaleta Maswali machache ili tupate kujua kama kweli tumeelewa ili tupate endelea na Ukumbusho Mwengine ambao utahusu. (NAJISI) Aina zake na Jinsi ya Kujitwaharisha na Hizo Najisi Nawashukuru sana kwa Ushirikiano wenu M/Mungu awabariki Tuzidi kuombeana Kheri ili tupate Radhi zake M/Mungu na tuupate Mwisho Mwema Inshallah MASWALI NAOMBA MYALETE KATIKA GROUP YENU YA KIJANA WA KIISLAM TANZANIA.MUNGU awabariki

No comments:

Post a Comment