Ewe Ndugu yangu katika Imani Kijana Mwenzangu Baada ya
kueleza katika Post iliyopita Maana ya FIQH ki Lugha na Maana ya Wanachuoni wa
Fani hii vile vile kutaja MISINGI YA FIQ-HI leo Inshallah tunaendelea katika
kueleza Maana ya Kila Msingi katika Misingi ya
Elimu hii ya FIQH.
1.QUR-AN
Qur-an Tukufu ni kitabu kilichokusanya maneno matukufu ya Mwenyezi Mungu alichoshushiwa Mtume wa mwisho, Nabii Muhammad kupitia kwa Malaika Jibril ili kiwe ni sheria na muongozo kwa wanadamu wote.
2.HADITH(SUNNAH)
Hadith ni tafsiri sahihi na ufafanuzi kamili wa Qur-ani Tukufu uliotolewa na Bwana Mtume kwa njia ya vitendo, maneno na "IQRAARI"."IQRAARI" ni kitendo cha Bwana Mtume kumuona mtu akitenda jambo fulani, kisha Mtume asitoe maelekezo yoyote ya kukemea au kukataza. Ukimya huu wa Mtume hutafsirika kuwa jambo lile linafaa kwani Mtume hawezi kulinyamazia jambo baya.
3.IJMAA3
Ijmaa3 ni kongamano na makubaliano ya wanazuoni wa kiislamu baada ya kuja Mtume juu ya jambo au suala ambalo halikuelezwa kwa uwazi ndani ya Qur-ani au hadithi
4.QIYAASI
Qiyaasi ni mizani ya kulipima jambo au suala ambalo halina ufafanuzi ndani ya Qur-ani au hadithi na jambo au suala lililotajwa ndani ya Qur-ani au Hadith, kwa kulingana sababu.
Kwa ufupi hizi ndizo maana nyepesi na za awali za misingi hii minne ambayo ndio chimbuko la elimu hii ya sheria ya Kiislamu, elimu ya FIQH.
Angalizo: Misingi hii Minne Miwili ya Mwanzo Qur an na Sunna Wanawachuoni wote wamekubaliana katika Misingi hiyo.
Ama Namba 3 - 4 Wanawazuoni wametofautiana katika Misingi hii na Mengine ambayo Inshallah Huenda tukakutana Nayo M/Mungu akipenda.
Inshallah Tutaendelea Na Faida za Elimu hii ya Fiqh

No comments:
Post a Comment