Monday, June 04, 2012

FAIDA ZA FIQH


FAIDA ZA FIQH
Tunaendelea na Ukumbusho wetu baada ya kueleza Maana ya kila Msingi katika Misingi Mikuu Minne ya Chimbuko au Asili ya Elimu hii ya Fiqh kwa Kukumbuka zaidi tuliitaja kuwa ni

1.Qur an
2.Sunna
3.Ijmaa3
4.Qiyassi

Leo tuna endelea katika kuangalia Baadhi ya Faida zipatikanazo kwa mwenye kuisoma Elimu hii ya Fiqh.
Kumbuka Ewe Kijana Mwenzangu kuwa Umuhimu na faida itokanayo na elimu hii ya fiqh unajidhihirisha katika maisha ya kila siku ya Muislamu, jamii na ummah mzima wa Kiislamu. Fiqh humsaidia Muislamu kujua:-

1.Maamrisho ya Mola wake, akayafuata ikawa ni sababu ya kupatia mafanikio ya Duniani na Akhera.

2.Makatazo ya Mola wake, akayaepuka ikawa pia ndio sababu ya kusalimika na maafa ya Duniani na Akhera.

3.Namna ya kutekeleza lengo la kuumbwa kwake ambalo ni ibada. Vipi na jinsi gani atamuabudu Muumba wake katika maisha yake yote.

4.Uhusiano wake na Mola wake, uhusiano wake na wanadamu wenziwe, uhusiano wa taifa na taifa jingine.

4.Halali na haramu. Fiq-hi ndio humbainishia ni lipi halali kutenda, kusema au kula na ni lipi haramu kutenda, kusema au kula.

5.Hukumu za makosa mbalimbali. Fiqh humuongoza Muislamu kutoa hukumu na adabu za makosa mbalimbali kuanzia yale madogo mpaka ya jinai.

Hizi ni baadhi ya faida zipatikanazo katika fani hii ya fiqh, Tumuombe M/Mungu atupe utambuzi zaidi katika Elimu hii na Elimu nyengine kwa Ujumla Hakika ya yeye Ndiye Mjuzi Pekee

No comments:

Post a Comment