Monday, June 04, 2012

HUKUMU YA SHERIA KATIKA FIQH


Asalaam Alaykum Warahmatu llahi Wabarakatu
Ndugu zangu wapendwa baada ya kuona Faida za elimu hii ya FIQH tunaendelea kwa uwezo wake M/Mungu na

HUKUMU YA SHERIA KATIKA FIQH
Baada ya kuona faida na umuhimu wa fiqh hatuna budi kujua hukumu ya shari3 katika elimu hii. Kila elimu katika Uislamu ina hukumu yake, elimu ya uchawi kwa mfano ni haramu.N.k

Elimu ya fiqh ni fardhi kwa muislamu kujifunza kwani kwa kupitia elimu ndiyo huweza kutekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Lakini ufaradhi huu unatofautiana baina ya mtu na mtu. Kwa mwengine huwa ni fardhi ya lazima kujua vipengele fulani na kwa mwengine huwa ni fardhi kifaaya(si ya lazima)

FARADHI YA LAZIMA:

Kujifunza, kuijua na kutumia elimu hii ya fiqh inakuwa ni faradhi ya lazima kwa kila Muislamu mwanamume na mwanamke katika mambo ya ibada ya kila siku, kwa mfano sala na funga. Kujua kutoa zaka, au kujua jinsi ya kuhiji wakati hana uwezo si fardhi ya lazima bali ni faradhi kifaaya, ama kwa mwenye uwezo ni fardhi ya lazima kujua elimu hizo.

Kwa mantiki hiyo hiyo, mwenye kufanya biashara ni fardhi ya lazima kujua vipengele vya kufanya biashara ndani ya fiqh ili biashara yake iwe kwa mujibu wa shari3 ya kiislamu na kutokwenda kinyume na Misingi na Kanuni ya Dini yetu.

FARADHI YA KUTOSHELEZEANA

Elimu hii inakuwa ni faradhi ya kutoshelezeana katika masuala ya mirathi, elimu ya ukadhi, elimu ya kutoa fat-wa na elimu nyingine zinazofanana na hizo. Sasa ikiwa ndani ya mji hakuna anayejua masuala ya mirathi, wakazi wote huwa na madhambi kwa kutojifunza elimu hiyo.
Huu ndio mgawanyo wa hukumu ya sheria kuhusiana na fani hii ya elimu ya fiqh.

HUKUMU ZA SHERIA YA KIISLAMU.

Kumbuka Ndugu yangu Mpendwa Kuwa Jambo lolote lile katika maisha ya kila siku ya Muislamu linaangukia kwa mujibu na mtazamo wa shari3 katika mafungu yafuatayo ya hukumu:-

1.Faradhi/Wajibu
2.Sunnah
3.Haramu
4.Mubah
5.Makuruuh

Hizi ndizo hukumu tano zinazoitawala sheria ya kiislamu Inshallah M/Mungu akipenda tutakuja tolea Maelezo Moja moja katika Hukumu hizo M/Mungu Mjuzi zaidi

No comments:

Post a Comment