Monday, June 04, 2012

JEE MTU AKITAKA KUWA MUSLAMU AMBAYE SI MUISLAMU NINI ANAPASWA AFANYE ?





Asalaam Alykum Ndugu zangu wapendwa katika Imani katika Uislam
Baada ya kujikumbusha Maana na Nguzo kuu Tatu Ambazo Ndio misingi ya DINI nayo ni UISLAM , IMANI , IHSANI, Leo Inshallah Tuangalie JEE MTU AKITAKA KUWA MUSLAMU AMBAYE SI MUISLAMU NINI ANAPASWA AFANYE ?
Kwa Mafundisho ya Kiislam Tunafundishwa katika Hadith za Mtume (S.A.W) Na kuamini kwamba kila mtoto anazaliwa hali ya kuwa tayari ni muislamu tokea tumboni mwa mama yake. Anabakia na Uislamu wake huo wa kuzaliwa mpaka anapofikia umri wa utu uzima (baleghe) hali ya kuwa na akili timamu. Katika umri huu ndipo anapoweza kuitumia akili na khiyari aliyopewa na Mola wake hapo sasa kwa wale wasiokuwa waislam ndio panapokuwa na Ubatizo N.k
M/Mungu anasema kwa wale wasio kuwa waislam :
“…………. BASI ANAYETAKA NA AAMINI (awe muislamu) NA ANAYETAKA NA AKUFURU (awe kafiri). HAKIKA TUMEWAANDALIA MADHALIMU (Makafiri) MOTO AMBAO KUTA ZAKE ZITAWAZUNGUKA …………” (
18: 29). Surat Al-Kahf

M/Mungu anauueleza Mfumo Dini ya Kiislam kuwa ni Mfumo asilia kusema: “BASI UELEKEZE USO WAKO KATIKA DINI ILIYO SAWA SAWA NDILO UMBILE ALLAH ALILOWAUMBIA WATU (yaani dini hii ya kiislamu inawafikiana barabara na umbo la binadamu). HAKUNA MABADILIKO KATIKA MAUMBILE YA VIUMBE VYA ALLAH. HIYO NDIYO DINI ILIYO YA HAKI, LAKINI WATU WENGI HAWAJUI” (30:30) Surat Ar - Rum

Kwa kufuata mfumo mwingine wa maisha (dini) ulio nje ya Uislamu ambapo atakuwa amejitia khasarani mwenyewe: “NA ANAYETAKA DINI ISIYOKUWA YA KIISLAMU BASI HAITAKUBALIWA KWAKE NAYE AKHERA ATAKUWA KATIKA WENYE KHASARA (kubwa kabisa)” (3:85).

Sasa kwa Mtu ambaye si Muislamu anapotaka kwa khiyari yake kurudi katika umbile lake la asili (Uislamu) anachohitajiwa kufanya kitu cha pekee kutamka hadharani shahada mbili na kuishi kwa mujibu wa shahada mbili hizo. ambazo Inshallah Tuzi Post baada ya Hii

No comments:

Post a Comment