Monday, June 04, 2012

MAANA YA SHAHADA MBILI


SHAHADA MBILI NI NINI?
Shahada mbili ni mkusanyiko wa matamko mawili ya ahadi anayoichukua kiumbe (mwanadamu) mbele ya Muumba wake na viumbe wenzake. Ambapo mtamkaji hula kiapo cha utii kwa Allah Mola Mwenyezi na Mtume wake katika maisha yake yote kwa kufuata maamrisho na makatazo yake.
SHAHADA YA KWANZA – TAMKO LA UTII KWA ALLAH:
“ASH – HADU AN LAA ILAAHA ILLAL-LAAHU”
Maana : “Ninakiri kwa moyo na kutamka kwa ulimi kwamba hapana afaaye kuabudiwa kwa haki ila Allah (Mola asiye na mshirika wala mwana)”

SHAHADA YA PILI: TAMKO LA UTII KWA MTUME WA ALLAH.
Ni mtu kutamka kwa moyo na ulimi:-
“WA ASH-HADU ANNA MUHAMMADAN ABDUHU WA RASUULUHU”
Maana: “Na ninakiri kwa moyo natamka kwa ulimi kwamba Muhammad ni mja na mjumbe wa Allah (kama alivyo Isa, Musa, Ibrahimu) Matamko mawili haya ya ahadi ndio tiketi ya kuingilia katika Uislamu baada ya mtu kujitoa mwenyewe. Mtu akiyatamka maneno haya tu tayari anakuwa muislamu tena na papo hapo anawajibika kuishi chini ya kivuli na mipaka ya shahada mbili hizo. Kwani kuishi kwa mujibu wa shahada mbili ndiko kutampa sifa ya kuwa muumini mbele ya Alah Mola Muumba wake na mbele ya viumbe (waumini) wenzake.

HILI NDIO NENO AMBALO ATALISEMA MTU ASIYEKUWA MUISLAM ATAKAPOTAKA KUREJEA KATIKA DINI YAKE YA ASILIA KAMA TULIVYO ELEZEA KATIKA POST ILIYOPITA Wamaa Taufiqh Illa Billah Wasalaam Alykum Warahmatullah Wabakatu WALLAH

No comments:

Post a Comment