Ewe Kijana Mwenzangu wa Kiislam Kaka yangu Mpendwa Dada
yangu Mpendwa Amka/Umeamka Nenda katafute Hakika kila kiumbe Dunia Ridhiki yake
imeshaandikwa toka kabla ya kuumbwa kwake na M/Mungu Mtukufu.
M/Mungu anasema katika
Qur an : Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humtengezea
njia ya kutokea.(2)
Na humruzuku kwa jiha(Upande) asiyo tazamia. Na
anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza
amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.(3) Surat At Talaaq Aya 2-3
ZINGATIA VITU VIKUU VIWILI ILI IWE WEPESI KWAKO KATIKA KULIFIKIA FUNGU LAKO.
1.UCHA MUNGU
2.KUMTEGEMEA M/MUNGU.
Kutoka kwa Sayyidna Ummar ibn Khatab Radhi za M/Mungu zimshukie juu yake anasema imepokelewa kwa Mtume (S.A.W) Rehma na Amani zaimshukie Juu yake anasema"Laiti kama Nyinyi (Wanaadamu)Mngelikuwa mnamtegemea M/MUNGU ukweli wa kumtegemea Angewapeni Ridhiki kama anavyo wapa Ridhiki Ndege wanarauka (Asubuhi/Alfajiri) wakiwa na Njaa na wanarejea Jioni wakiwa wameshiba"Imepokewa Hadithi na Imam Ahamd na Tirmidh.
ANGALIZO
kumtegemea M/Mungu ni kutoka na kutafuta
na si kusema Inshallah Mungu atatoa au ataleta Enyi Vijana wenzangu tutafute
sababu katika kulipata Fungu letu la Ridhiki ya kila siku katika kufanya kazi
yeyote ila iwe na Uhalali Ndani yake Na Inshallah M/MUngu atatusaidia Nawatakia
kazi Njema M/Mungu Ndiye Mjuzi zaidi
No comments:
Post a Comment