Tuesday, June 05, 2012

MAANA ISTIHAADHA





MAANA ISTIHAADHA

Istihaadha ni damu ya ugonjwa damu hii hutoka katika mshipa ulio ndani kabisa ya tumbo la uzazi.

Damu hii hutengua udhu lakini haiwajibishi josho kama ilivyo kwa
damu ya hedhi.
Vile vile damu hii haitoi fursa ya kuacha kuswali na kufunga.

Mwanamke mwenye maradhi haya ya Istihaadha anatakiwa aioshe damu na afunge utepe mahala itokapo kisha atawadha na halafu aswali.

Imepokelewa riwaya kutoka kwa Fatmah Bint Abiy Hubaysh M/Mungu amuwiye radhi kwamba yeye alikuwa akitokwa na istihaadha Mtume (S.A.W) akamwambia "Ikiwa ni damu ya hedhi, basi itakuwa ni damu nyeusi ijulikanayo.
Itakapokuwa hivyo basi acha kuswali, ikiwa ni nyingine basi Tawadha na uswali, hakika si vingenevyo huo ni mshipa ". Kama alivyosema Mtume imepokelewa Abu Daawoud.

NIFASI
Ama damu ya Nifasi Ni damu ambayo hutoka Baada ya Uzazi (Kujifungua).

Zote hizi Damu Mbili zitapo Mtokea Mtu zina Muwajibisha Kukoga Josho Kubwa (Josho la Faradh/Wajib ) tukisema Damu Mbili Nakusudia Hedhi na Nifasi ama Damu isiyo kuwa hiyo Rejea hapo Juu katika Kipengele cha Istihaadha.

ANGALIZO:-
Ziko Tabia za Baadhi ya watu Baada ya Kumaliza au kukata Damu ya Uzazi hutafuta Maalim kwa Ajili ya KumTwaharisha Hii si katika Dini ya Uislam Maelekezo ya Kukoga JOSHO KUBWA REJEA POST JINSI YA KUKOGA JANABA ILA KUNA BAADHI YA MAMBO MACHACHE HUENDA YA KAZIDI KATIKA HALI YA KUJISAFISHA SAIDIANENI WENYEWE KWA WENYEWE WANAWAKE WA KIISLAM KATIKA KUFUNDISHANA MEMA MNAPOKUTANA KATIKA SHUGHULI ZENU ZA WANAWAKE TU.

Ongezo katika Josho la Hedhi inapasa Misuko ya Nywele ifuliwe kutokana Josho hili linakuwa kwa Mwezi Mara Moja tu kwa Mwezi.

Ndugu zangu Mtaniwia Radhi lengo ni kukumbushana M/Mungu Ndiye Mjuzi.

No comments:

Post a Comment