Tuesday, June 05, 2012

Mambo ambayo Ni Haramu kufanya Mtu ambaye yupo katika hali hiyo ya Siku zake (HEDHI)





Ndugu zangu katika Imani Baada ya Kueleza Maana ya Hedhi na mengineyo InshaALLAH tunaendelea na kutaja Mambo ambayo Ni Haramu kufanya Mtu ambaye yupo katika hali hiyo ya Siku zake (HEDHI).

1.Kuswali

2.Kutufu Al-Kaaba

3.Kugusa Msaafu (Qur an)

4.Kuubeba Msaafu (Qur an)

Rejea Dalili ya Mwenye Janaba.

5.Kukaa msikitini

6.Kusoma Qur an

7.Kufunga Funga ya Faradhi au Sunna

Angalizo:-
Atalipa mwenye hedhi Funga iliyompita katika kipindi cha hedhi baada ya kusafika/Twaharika kwake.
Ama Kuhusu Swala hatakiwi kulipa zilizompita katika kipindi yupo katika Siku zake Mwanamke.

8.Kuachwa kwa Mwanamke (Kupewa Talaka )

9.Kupita Msikitini

Angalizo:-
Kupita msikitini kwa sababu damu ni najisi na ni haramu kuuchafua msikiti kwa najisi na uchafu mwingineo Ikiwa mwanamke atajiaminisha kutokuuchafua msikiti basi anaweza kukatiza na kupita msikitini.

10.Haifai Kuingiliwa kwa Maana kufanya naye tendo la ndoa Mwanamke ambaye yupo katika Siku zake

Dalili
M/Mungu anasema " BASI JITENGENI NA WANAWAKE WAKATI WA HEDHI (zao) WALA MSIWAKARIBIE MPAKA WATWAHARIKE. WAKISHAKUTWAHIRIKA BASI WAENDEENI
KATIKA PALE ALIPOKUAMRISHENI ALLAH…" Qur an Suratul Baqara Aya 222

Kusudio la kujitenga na wanawake ni kuacha kuingiliana nao kimwili.

Kwa Ibara Maarufu katika FIQH Madh hab haifai kwa Mwanamke aliye katika siku zake kustarehe Nae sehemu zilizo kati ya Kitovu na Magoti.
Tutakuwa tumefika Mwisho wa Ukumbusho unaohusu Hedhi Nipende kukumbusha Zaidi haya Ni Machache katika Mengi ambayo tunatakiwa tufahamu hivyo basi hii iwe Mwanzo na Chachu ya kusaka Walimu na Masheikh katika kutaka Jua / Uliza Mengi katika FIQH na Mambo ya Dini yote Tusitosheke na Post za Kijana Wa Kiislam Tuwe karibu Na Masheikh zetu tupate Tambua mengi TUTAENDELEA NA BAADHI YA MAREJEO YA NUKTA MUHIMU NAWASHUKURUNI

No comments:

Post a Comment