Tuesday, June 05, 2012

MAANA YA HEDHI

Ndugu yangu katika Imani kama utakumbuka katika Post zilizopita tumetaja Mambo ambayo yanapo Mpata Mtu inamlazimu kukoga Josho la Waajib Faradh Alhamdullilah
tumeeleza Jambo Moja ambalo Ni Janaba Jinsi linavyo patikana na Jinsi ya Kujitwaharisha kwake InshaAlla leo tutaendelea na Baki ya Mambo mengine na tutazungumzia Hedhi Maana yake na Muda wake.

MAANA YA HEDHI

Neno Hedhi Ki Lugha Maana yake ni KUCHURIZIKA.

Kwa Mtazamo wa Watu wa Elimu ya Sharia ni DAMU YA MAUMBILE yaani damu hii ni
sehemu/ni katika jumla ya maumbile ya Mwanamke,
Mwanamke kaumbwa hivyo kwa lengo maalum.
Damu hii hutoka ndani kabisa ya tumbo la uzazi kila mwezi baada ya mwanamke kutimiza kwa uchache umri wa miaka tisa

DALILI
Dalili na ushahidi wa Kuwajibishwa Mwenye kutokwa Damu hiyo Kuji Twaharisha Kukoga Josho Kubwa.

Dalili katika Qur an M/Mungu anasema
"NA WANAKUULIZA JUU YA HEDHI , WAAMBIE HUO NI UCHAFU. BASI JITENGENI NA WANAWAKE WAKATI WA HEDHI (zao). WALA MSIWAKARIBIE MPAKA WATWAHARIKE.
WAKISHATWAHARIKA BASI WAENDEENI KATIKA PALE ALIPOKUAMRISHENI ALLAH…" Qur an Suratul Baqara Aya 222.

Dalili katika Sunna

Mtume(S.A.W) anasema Imepokelewa Hadith na Fatmah Bint Abiy Hubayshi M/Mungu amuwie Radhi Mtume anasema "Itapokujia hedhi , basi acha kuswali na itakapomalizika (kutoka) basi ikoshe damu (Twaharisha) na uswali"kama alivyosema Mtume Bukhaari na Muslim.

MUDA WA HEDHI

Kusudio la ibara (Muda wa hedhi) kipindi ambacho mwanamke hutumika
yaani huwamo hedhini.
Kipindi hiki tunaweza kukigawa katika sehemu tatu.

Kipindi kifupi
Kipindi kirefu
Kipindi cha katikati ( Ada )

KIPINDI KIFUPI

Huu ndio muda wa chini kabisa wa kutoka damu ya hedhi hiki ni kipindi cha masaa ishirini na nne (24).
Hii inaamaanisha kuwa mwanamke anaweza kuingia hedhini mchana na usiku wake tu kisha damu ikakatika.

KIPINDI KIREFU

Huu ndio muda wa juu kabisa wa kutoka damu ya hedhi
Hiki ni kipindi cha siku kumi na tano (15) mchana na usiku

KIPINDI CHA KATIKATI
Huu ndio muda wa ada na desturi kwa wanawake walio wengi, yaani wanawake wengi hutumika katika kipindi hiki. Huu ni muda wa siku sita au saba

Muda wa chini wa Twahara, yaani kipindi cha chini ambacho mwanamke anakuwa katika twahara ni siku kumi na tano(15).
Hakuna ukomo ( limit ) wa wingi wa Twahara kwani inawezakana kabisa mwanamkeasipate hedhi kwa muda wa mwaka miaka miwili au miaka kadhaa na hili limethibiti kwa majaribio

Mwanamke atakapoiona damu chini ya kipindi kifupi cha hedhi yaani chini ya masaa ishirini na nne au aliiona damu baada ya kule kipindi kirefu cha hedhi yaani baada ya siku kumi na tano, damu hii itazingatiwa kisharia kuwa ni damu ya ISTIHAADHA (Ugonjwa) na sio damu ya hedhi.

Hii Ndio Damu ya Hedhi ambayo Inamuwajibisha Kukoga Josho Kubwa Pale Inapo dhihiri kwake InshaAllah tuendelea kueleza Nini Istihaadha (Damu ya Ugonjwa ) na yanayo Pasa kwa Damu hiyo. M/Mungu Ndiye Mjuzi

No comments:

Post a Comment