Tuesday, June 05, 2012

Mambo ambayo Ni Haramu kwa Mtu Mwenye Janaba





Ndugu yangu Mpendwa katika Imani InshaAllah kwa uwezo wa Mungu Baada ya kuona Jinsi ya Kukoga Janaba kiukamilifu leo Tunaendelea na Post zetu kwa kuangalia Mambo ambayo Ni Haramu kwa Mtu Mwenye Janaba

1.Kuswali swala ya fardhi au ya sunna
Hii ni kwa mujibu wa kauli ya M/Mungu Mtukufu: "ENYI MLIOAMINI! MSIKARIBIE SWALA, HALI MMELEWA MPAKA MYAJUE MNAYOSEMA WALA HALI MNA JANABA ISIPOKUWA MMO SAFARINI ( mnapita njia ) MPAKA MKOGE…" Qur an Suratil Maidah Aya 43.

Maelezo ya Aya Kwa Ufupi Na Kusudio la Neno Swala.

Kusudio la neno SWALA katika aya hii ni MAHALA PA KUSWALIA ( msikiti ) kwa sababu kupita njia hakupatikani ndani ya Swala.
Ikiwa mwenye janaba anakatazwa kupita msikitini basi kukatazwa kuswali ni aula zaidi.
Ibn Umar Mungu amuwie Radhi amesema : Hakika nimemsikia Mtume (S.A.W) akisema " Haikubaliwi swala bila ya twahara".Kama alivyosema Mtume Hadithi Imepokelewa na Imam Muslim

Twahara iliyotajwa katika hadithi ni pamoja na Twahara ya hadath ndogo na Janaba ( hadathi kubwa ) Hadathi hii inafahamisha uharamu wa kuswali kwa mwenye hadath zote hizo hadathi ndogo na hadathi kubwa(Janaba).

2.Haifai kwa Mwenye Janaba Kutufu Al-Kaaba

3.Haifai kwa Mwenye Janaba Twawafu ya Nguzo/fardhi au ya sunna hii ni kwa sababu Twawafu iko katika daraja ya Swala kwa hiyo nayo imeshurutizwa Twahara kama ilivyo kwa Swala.

4. Kugusa Msaafu (Qur an )

5. Haifai kwa Mtu Mwenye Janaba Kuubeba Msaafu (Qur an )

6. Haifai kwa Mtu Mwenye Janaba Kukaa Msikitini

7. Kusoma Qur-ani. Amesema Mtume Muhammad (S.A.W) " Asisome mwenye hedhi wala mwenye janaba chochote katika Qur-ani".Kama alivyosema Mtume Imepokelewa na Tirmidhiy

ANGALIZO: INAFAA kwa mwenye Janaba kuisoma Qur an moyoni bila ya kuitamka kwa ulimi kama ambavyo inafaa kuutazama Msahafu bila ya kuushika vile vile Inafaa kusoma Dhikri/Nyiradi za Qur-an kwa kukusudia ile Dhikri na sio Qur an .
Mfano Dhikri ya Qur-ani ni kama kusema :-

"RABBANAA AATINAA FID-DUN-YAA HASANATAN WAFIL AAKHIRATI HASANATAN WAQINAA ADHAABAN-NAAR” Qur an Suratul Baqarah aya ya 201.
Kufaa huku kwa kusoma hii kwa Mtu Mwenye Janaba kwa kuikusudia aya hii kama dua na sio Qur an Mfano Mwengine anapopanda Kipando (chombo cha usafiri)
"SUB-HANNAL-LADHIY SAKHARA LANNA HAADHA WA MAA KUNNAA LAHU MUQRINIYN") Qur an Suratil Az- Zukhruf aya 13 kwa kuisudia hii kama dua na sio dhati ya Qur-ani yenyewe.
Mpaka Hapa Tutakuwa InshaAllah Tumefunga Kipengele cha Janaba Na InshaAllah Post ijayo Tutazungumzia Baaki ya Vitu Vingine ambavyo Vinampasa Mtu Kuoga Josho Kubwa Nawashukuruni Saana M/Mungu ndiye Mjuzi

3 comments:

  1. Nambari ya kwanza ... reference yake haiko sawa ...surat maida aya ya 43 haizungumzi jambo hilo tafadhali angalieni kwa uangalifu na murekebishe.

    Napia suala jee inafaa kusikiliza QUR-AN Hali unajanaba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shukran Kaka Usahihi ni suratu Nisaa Aya 43

      Delete
  2. Shukran kwa Ukumbusho Rejeo la Usahihi ni suratul Nisaa Aya ya 43.

    ReplyDelete