Tuesday, June 05, 2012

NAMNA YA KUCHUKUA UDHU


Ewe Ndugu yangu katika Imani Kama tulivyosema kuwa Ukumbusho Ujao utakuwa ni namna ya kuchukua Udhu baada ya kuona Maana ya Udhu, Hukmu za Udhu na Dalili zake,Ubora na Fadhila za Udhu naonelea ni Bora tuuishi katika hii hii Siku ya Ijumaa kwa Kuangalia 
NAMNA YA KUCHUKUA UDHU kutokana na Umuhimu wa Udhu katika Maisha yetu ya kila Siku ya Ibada .

1.NAMNA YA KUCHUKUA UDHU
Ikiwa unachukua Udhu kwa kutumia chombo kama vile birika/Kopo basi ni vyema kama inawezekana liwe upande wako wa kulia na kama unatumia bomba basi fungua bomba lako na fuata Hatua zituatazo:

1.Anza kukosha vitanga vya mikono huku ukisema BISMILLAHIR-RAHMANIR-RAHIYM. Mara 3.

2.Baada ya kuosha vitanga vya Mikono, tia maji mdomoni na Sukutua mara 3.

3.Pandisha maji puani na safisha tundu za Pua mara 3

4.Osha uso wako ukianzia Kuanzia maoteo/mameleo ya nywele za kichwa mpaka mwisho wa kidevu kwa urefu na toka ndewe moja ya sikio hadi nyingine kwa upana.

Angalizo

Pindi unapokuwa unakosha ndio sehemu ambayo unatakiwa ulete/tia Nia na Mahala pake Moyoni ama kuitamka Nia ni Sunna kama tulivyoelekezwa na walimu wetu katika Fiqh.
Matamshi ya Nia Ni kama yafutayo :
NAWAYTU RA-AL HADATH (Nanuia kuondosha Hadathi/uchafu)
au
NAWAYTU FARDHAL-WUDHU(Nanuia kutekeleza Wajibu wa Udhu) au maneno yenye kufanana na hayo ma pia Uso huoshwa mara 3.

5.Kuosha mikono Miwili ukianzia mkono wa kulia kisha Mkono wa kushoto. kumbuka kuwa na Mikono Nayo Huoshwa mara 3.

6. Kupaka Maji sehemu katika Kichwa Mara 3.

7.Kukosha masikio , ndani na nje mara 3.

8.Ni hatua ya Mwisho nayo ni kuosha Miguu ukianzia wa kulia kisha wa kushoto Mara 3.

Kwa utaratibu huu udhu wako utakuwa umekamilika na hivyo kumaanisha kuwa sasa unayo rukhsa ya kusimama na kuzungumza na M/Mungu ndani ya swala.
Ewe Ndugu yangu Mpendwa katika Imani kumbuka kuufuta Utaratibu huu kwa Namba kama tulivyo elekeza ili kuenda kama alivyotuelekeza Mtume(S.A.W) kutoka kwa Maswahaba zake
Inshallah Nina Imani Mpaka Hapa Utakuwa umepata Muangaza fulani katika Uchukuaji wa Udhu Inshallah Ukumbusho unaofuata utahusu Nguzo za Udhu

1 comment: