Tuesday, June 05, 2012

Sharti za kusihi udhu





Ndugu zangu katika Imani Baada ya Kueleza Sunna za Udhu leo kwa Uwezo wake Allah Tunaendelea kueleza Sharti za Kusihii huo Udhu.

Sharti za kusihi udhu
Maana yake ni mambo ambayo mwenye kutawadha aya hakikishe kwanza kabla hajaanza kutawadha, ili udhu wake uweze kusihi na kukubalika kisharia. Miongoni mwa sharti muhimu kabisa za udhu ni kama zifuatazo :

1.Kutokuwepo kizuizi kinachoweza kuzuia maji wakati wa kutawadha kuuifikia ngozi, Mfano wa Kizuizi kama mafuta mazito ya mgando, ute wa mshumaa, rangi ya lami, na vitu vyenye kufanana.

2.Lisimpate mwenye kutawadha wakati wa kutawadha kwake jambo lenye kuubatilisha na kuutengua udhu wake, kama vile kutokwa na kitu katika mojawapo wa tupu mbili.

3.Maji ya udhu yawe ni TWAHARA na yenye kufaa kutumika kwenye udhu.

4.Kutakata mwanamke kutokana na damu ya hedhi na nifasi, kwani udhu hausihi wala kumpasa mwanamke aliye katika hedhi au nifasi mpaka atakapotahirika.

5.Uislamu wa mwenye kutawadha, kwani udhu si wajibu na wala hausihi kwa asiyekuwa muislamu, hata kama atafata taratibu zote za udhu.

6.Kusiku wepo juu ya kiungo cha udhu kitu chochote kinachoweza kuharibu mojawapo ya sifa tatu za maji, ambazo ni tamu (ladha), rangi na harufu. Vitu hivi ni pamoja na vumbi la mkaa, chokaa, Cement N.k

Hizi Ndizo Sharti za Kusihi Udhu.
Maelezo zaidi kuhusu Sharti ya 6 Uislam Ndiyo Nguzo ya Kwanza katika Kusihi Ibada zote Iwe Swala, Funga , Hijja na Nyenginezo katika Ibada hazitosihii ibada ya Funga na tulizozitaja kwa Mtu asiyekuwa Muislam hata kama atakuwa anafunga Sharti la Uislam Lizingatiwe ili kupata kusihi kwa Ibada yake.
Mpaka hapo Ndugu yangu Tutakuwa tunaenda sawa na Inshallah Tuzidishe Maombi na Ibada katika Mwezi huu wa Rajaab kuelekea Shaaban na kufikia Mwezi Mtukufu wa Ramadhan Maandalizi Bora Ni Kujikurubusha zaidi kwa Mungu na Kumuomba M/Mungu kufika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan Haya Ndio Mapokezi Sahihi ya Mja mwema

No comments:

Post a Comment