Ndugu katika Imani Baada ya Kueleza Sharti za kusihi Udhu Inshallah yapo Mambo ni karaha kufanya kwa MTU mwenye kuchukua Udhu Baadhi ya Mambo hayo ni :-
YALIYO KARAHA KATIKA UDHU
1.Ni karaha kwa mwenye kutawadha kuacha sunna yeyote miongoni mwa sunna za Udhu tulizozitaja kwa sababu kuacha kuzitekeleza suna hizo kutampelekea mtu huyo kukosa Thawabu, na muislam wa kweli siku zote hupupia kuitekeleza ibada yake kwa ukamilifu na kwa namna ilivyofundishwa na mwenyewe Bwana Mtume (S.A.W)
2.Ni karaha kuyatumia maji kwa israfu (fujo)
3.Ni karaha kutanguliza kuosha mkono/mguu wa kushoto kabla ya mkono/mguu wa kulia , kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na alivyotenda Bwana Mtume (S.A.W).
4.Ni karaha kukausha/kufuta viungo vya udhu kwa kutumia leso/taulo.
Ukaraha huo utaondoka kwa udhuru kama vile baridi kali, hapo itakuwa si karaha.
5.Ni karaha mtu kuoshwa viungo na mtu mwingine bila ya kuwa na udhuru ukubalikao kama ugonjwa.
Hili limefanywa kuwa ni karaha na sharia kwa sababu ndani yake mna aina ya kibri na ubwana, vitu ambavyo Uislam Unavipinga.
6.Ni karaha kwa aliyefunga kuyapeleka ndani sana maji katika kusukutuwa na kupandisha maji puani.
Hii ni kwa sababu ya kuchelea kufika Maji kooni na kusababisha kuharibika Funga yake.
Amesema Mtume (S.A.W) “ Na balighisha ( yapeleke maji ndani sana ) katika kupandisha maji puani , ila ukiwa umefunga ( usibalighishe )” Kama alivyosema Mtume Imepokelewa na Abuu Daawoud.
TANBIIH : Ikiwa imekatazwa kubalighisha katika kupandisha maji puani kwa mfungaji, basi kubalighisha katika kusukutua ni bora zaidi kukatazwa.
Inshallah Post ifuatayo itakuwa Vitenguzi vya Udhu kwa Uwezo wake Allah
No comments:
Post a Comment