Tuesday, July 30, 2013

AKHERA NI BORA KULIKO DUNIA

Tunapokuwa tuna furahia Maisha kwa kuwa na Gari nzuri , Nyumba Nzuri , Kitanda kizuri , Simu Nzuri ya HTC , Blackberry , Laptop za Model tofauti , Kadi za ATM katika Benki tofauti na Uwezo wa kubadili chakula cha Kila aina  tutakayo TUKUMBUKE kuilinda FURAHA HIYO YA HAPA DUNIANI NA KESHO AKHERA KWA CHUMO LILO HALALI.

Bora kutembea na Miguu, Baskeli , Kulala katika Nyumba isiyo na Umeme na kutumia Simu ya Tochi kuishi bila ya kuwa na ATM Card za Benki TUKUMBUKE  kuwa Chumo la halali ni Bora kwa %100 kuliko kuwa na FURAHA AMBAYO CHANZO CHAKE NI MALI ZA HARAMU.

AKHERA NI BORA KULIKO DUNIA 

Ewe M/Mungu tunakuomba tujaalie Rizki za halali na tufanye wenye kutosheka na kidogo tujaalie Dunia iwe kwa Mikono yetu na wala isiwe kwa Mioyo yetu Tusamehe Makosa yetu na Zipokee Dua zetu . Amiin

No comments:

Post a Comment