Ndugu zangu wapendwa tukumbuke kwamba Funga iko na Fadhila Nyingi sana Soma Hadithi zifuatazo ili tupate kujikumbusha Miongoni mwa Fadhila za Funga.
Zimepokewa Hadithi nyingi sana zinazoelezea fadhila za funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, miongoni mwa hadithi hizo ni hadithi zifuatazo:
1- Amesema Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani " Mwenye kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa imani na kutarajia malipo (toka kwa M/Mungu Mtukufu (aliyetakasika na kutukuka ) husamehewa madhambi aliyoyatanguliza". kama alivyosema Mtume Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani hadithi imepokewa na Maimamu wawili Bukhari na Muslim.
2- Amesema Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani " Kila amali (Matendo) ya mwanaadamu (aifanyayo) ni yake, wema (mmoja) hulipwa kwa mfano wake mara kumi mpaka mara mia saba, isipokuwa funga, hakika ya funga ni Yangu mimi, na Mimi najua namna gani Nimlipe kwa funga hiyo, ameacha matamanio yake na chakula chake na kinywaji chake kwa ajili Yangu, mfungaji ana furaha mbili, furaha wakati wa kufutari kwake na furaha nyengine pale atapokukutana na Mola wake. Harufu yakinywa cha mfungaji inapendeza zaidi kwa M/M ungu kuliko harufu ya miski ". Imepokelewa hadithi na Imamu Bukhari na Muslim.
3- Hufungiwa ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Mashetani kama alivyosema Mtume katika Hadithi ambazo tumeshazitaja katika Darsa zetu zilizopita.
4-Ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hufunguliwa Milango ya Peponi na hufungwa Milango ya Motoni.
Amesema Mtume (S.A.W) " Unapoingia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hufunguliwa Milango ya Peponi na hufungwa Milango ya Motoni hutiwa Macheni/Minyororo Mashetani " kama alivyosema Mtume Hadithi Imepokelewa na Imamu Bukhari.
5-Ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kunapatikana Usiku wa Cheo Usiku wa LAYLATUL QADIR Ubora wake ni zaidi ya Miezi 1000.
6- Ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuna Saa ambayo Mja akiomba kwa Mola wake Dua zake hazirudi patupu na tumeusiwa sana kuomba Dua wakati pale tunapo futuru .
Ndugu zangu wapendwa hizi ni katika chache ya Fadhila za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni hasara kwetu kama tutaudiriki Mwezi huu na ukaisha bila ya kupata nao faida.
من لم يربح في هذا الشهر، ففي أي وقت يربح
Mtu ambaye hatopata faida katika Mwezi huu wenye Nyingi Fadhila Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Wakati gani Mwengine atapata faida.
No comments:
Post a Comment