Monday, July 29, 2013

ITIKAFU NA MAANA YAKE NA DALILI ZAKE .

ITIKAFU NA MAANA YAKE NA DALILI ZAKE .

Maana ya Itikafu Ki - Lugha ni Kushikamana na kitu na kuizuia nafsi kwa ajili ya kitu hicho sawa kitu hicho kiwe ni kizuri au kibaya.
Dalili
M/Mungu Anasema katika kumuelezea Nabii Ibrahimu pindi alipo kuwa akimsimamishia hoja baba yake na watu wake dhidi ya kuabudia masanamu "Alipo mwambia baba yake na watu wake: Ni nini haya masanamu mnayo yashughulikia kuyaabudu? ".
Qur an Suratil Anbya Aya 52.

Ama Maana ya Itkafu Upande wa Ki - Sharia na Ndio Kusudio letu

Kushikamana na Msikiti na kukaa ndani yake pasina ya kutoka kwa ajili ya kujikurubisha(kuwa karibu) kwa M/Mungu Mtukufu .

Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu ziwe juu yake alikuwa akikaa itikafu katika kila Mwaka ndani ya kumi la mwisho la Ramadhani na Mwaka alio fariki alikaa itikafu muda wa siku ishirini Kama ilivyo pokelewa na Bukhari.

Vile vile Maswahaba wa Mtume na Wake zake walikaa nae itikafu na walikaa Itikafu baada ya mtume kufariki.

Ibada hii ya Itkafu imekokotezwa sana katika kumi la Mwisho la Ramadhani kwa Ajili ya Ku utafuta Usiku wa Cheo (LAYLATUL - QADIR) ambao unapatikana katika Mwezi 21,23,25,27,29.

Wanawazuoni wengi wameichagua na kumili katika siku hii ya Mwezi 27 na M/Mungu Ndiye Mjuzi zaidi wa Siku hiyo.

VIGAWANYO VYA ITIKAFU

Itikafu imegawanyika Sehemu mbili
1.Itikafu ya Sunna
2.Itikafu ya wajibu.

Itikafu ya Sunna ni itikafu ambayo Mja anajitole kwa huko kukaa kwake itikafu, kwa ajili ya kujikurubisha kwa M/Mungu na kujipatia thawabu.

Vile vile kwa ajili ya kumuiga Menendo wa Mtume Muhammad (S.A.W) Rehma za na Amani zimshukie Juu yake.

Muda wa Ibada wa Sunna hii imetiliwa Mkazo sana katika Kipindi hiki cha Ramadhani.

ITKAFU YA WAJIB
Ni itikafu ambayo Mja kaji wajibisha yeye mwenyewe.

Nayo inakuwa ima kwa Nadhiri ambayo haijaegemeshwa juu ya jambo lolote, Mfano: Nimetia nadhiri kwa ajili ya Allah kwa kukaa itikafu siku tatu.
Au inakuwa kwa nadhiri inayokuwa imeegemeshwa juu ya jambo fulani, Mfano:Iwapo Allah atamponya Mgonjwa wangu nitakaa itikafu kwa ajili ya Allah Muda wa siku moja.

Dalili
Mtume (S.A.W) Rehma za M/mungu zimshukie juu yake na Amani anasema "Yule atakaye tia Nadhiri ya kumtii Allah basi na amtii) Kama alivyosema Mtume hadithi imepokelewa na Bukhari.

Ndugu yangu katika Uislam huu Ni Mwanzo na IshaAllah kwa uwezo wake Allah tutakuwa ni Mwenye kuendelea na Maelezo ya Ibada hii ya Itkafu kwa uwezo wake Muumba.

Dua zenu za kheri msitusahau M/MUNGU azipokee funga zetu na Ibada zetu kwa Ujumla.Amiin ...

Na : Ghalib N Monero l Azhariy .

No comments:

Post a Comment