Tuesday, July 30, 2013

NASAHA ZA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Ndugu zangu Waislam
Tukiwa tupo tunaendelea na Ibada hii ya funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani tukumbuke kuwa kuna Mambo ambayo tunatakiwa tuyafanye kwa wingi na vile

vile kuna Mambo tunatakiwa tujiepushe Nayo.

AMBAYO TUNATAKIWA KUJIEPUSHA NAYO KATIKA MWEZI HUU NA BAKI YA MIEZI MINGINE.

1.Tabia Mbaya na maneno maovu Mfano wa kusengenya, kusema uongo n.k (Mwezi huu sana na baki ya miezi ).

2.Kulala sana kwani kulala huko kunatupotezea Fursa za kufanya Ibada ya Kusoma Qur an na Ibada Nyenginezo (Mwezi huu sana na baki ya miezi ).

3.Kupoteza wakati mwingi katika michezo na maongezi yasiyo na faida Vijiweni kwa

Kucheza Bao,

Karata na kuacha kuutumia wakati huo katika kazi na ibada mbali mbali Mfano kuhudhuria Darsa Misikiti kipindi cha Swala ya Alasiri au kwa Mujibu wa Ratiba za Masheikh wasimamizi wa Darsa hizo (Mwezi huu sana na baki ya miezi ).

4.Kuacha kula daku au kuchelewa kufuturu (Mwezi huu ).

5.Kufanya israfu katika vyakula na vinywaji wakati wa kufutari tukumbuke kwamba kuna wenzetu wengi nao wanahitajia Vyakula hivyo na Viywaji hivyo hakuna haja ya Israfu na kufanya Fujo katika Chakula (Mwezi huu ).

6.Kuacha kuswali Swala ya Tarawekhe ambayo ni Sunna inayopatikana Mwezi wa Ramadhani tu (Mwezi huu ).

Ndugu zangu wapendwa haya ni katika Mambo ambayo Mfungaji anatakiwa ajiepushe nayo zaidi katika Kipindi hiki cha Mwezi wa Ramadhani na Muda wake wote wa Maisha yetu .

Tumuombe M/Mungu kwa Ujumla azipokee Ibada zetu na azikubali Funga zetu Amiin ...

No comments:

Post a Comment