HAKIKA UMBO LA KILA MMOJA WENU LINAKUSANYWA KATIKA TUMBO LA MAMA YAKE.
Kutoka kwa Abu Abdur-Rahman Abdullaah Ibn Masu'ud Radhi za M/Mungu zimshukie Juu yake alisema: Mtume Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani naye ndie mkweli , anae sadikiwa alitueleza haya:
Hakika
umbo la kila mmoja wenu linakusanywa pamoja katika tumbo la mama yake
kwa muda wa siku arubaini, ikiwa katika hali ya mbegu, baadaye tone la
damu kwa muda kama huo, tena huwa ni kipande cha nyama kwa muda kama
huo, tena hupelekwa Malaika anaempulizia pumzi za uhai na anaamrishwa
mambo manne: kuandika rizki yake, maisha yake, amali yake na akiwa
atakuwa (mtu) mbaya au mwema. Kwa Allaah ambaye hakuna Mungu isipokuwa
Yeye, mmoja katika nyinyi hufanya vitendo vya watu wa peponi mpaka
baina yake na pepo ikawa dhiraa na kile kilichoandikwa kikathibiti
akafanya amali ya watu wa motoni akaingia motoni. Na mmoja katika
nyinyi hufanya amali ya watu wa motoni mpaka baina yake na moto ikawa
dhiraa, na hapo kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya amali ya watu
wa peponi akaingia peponi.
Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim.
------------------------------------------------------------------
"إن أحدكم يجمع في بطن أمه"
عن
أبي عبْدِ الرَّحْمن عبدِ الله بنِ مسعودٍ رضي الله عنه قال: حدَّثَنا
رسولُ الله صلى الله عليه وسلم وهُوَ الصَّادقُ المَصْدوق: إنَّ
أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ في بَطْنِ أُمِّه أرْبعينَ يوْماً نُطْفَةً،
ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذلك، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذلك،
ثُمَّ يُرْسَلُ إليه المَلكُ فَيَنْفخُ فيه الرُّوحَ ويُؤمَرُ بأرْبَعِ
كلماتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ وأَجَلِهِ وعَمَلِهِ وشَقيٌّ أو سَعيدٌ،
فَوَاللهِ الَّذي لا إله غَيْرُهُ إنَّ أَحَدَكُمْ ليَعْمَلُ بعَمَلِ أهْلِ
الجَنَّةِ حتى ما يكُونَ بَيْنَهُ وبَيْنَها إلا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ
عَليْه الكِتابُ فَيَعْمَلُ بعَملِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُها. وإنَّ
أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهل النَّارِ حتى ما يَكُونَ بَيْنَهُ
وبَيْنَها إلا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكتابُ، فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ
أهل الجنَّةِ فَيَدْخُلُها))
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ
No comments:
Post a Comment