SOMA UJUMBE HUU MPAKA MWISHO MUHIMU HUTBA NYINGI ZA LEO ZIMEZUNGUMZIA HILI ...
Zakkatul Fitri
Ndugu yangu kumbuka kwamba kutoa Zakatul Fitri ni Wajibu kwa kila
Muislam,Mwanamume, Mwanamke,Mkubwa, Mdogo, Muungwana (huru) au Mtumwa).
Inapasa kwa Muislam ikiwa atakuwa na uwezo wa kumiliki chakula na ziada
siku ya Iddi na Usiku wake Itampasa atoe yeye na wale ambao wako Chini
yake Kimalezi na Ungalizi.
Ikiwa Mtu anajitegemea Mwanamke / Mwanaume italazimika wao wenyewe kujitegemea katika kutoa Zakkah hizo.
Wakati wa kutolewa Zakkah hiyo Inatakikana itolewe Zakkatul Fitri kabla
ya Swala ama itakayo tolewa baada ya swala haiesabiki kuwa ni Zakkatul
Fitri bali Ni Sadaka kama Sadaka Nyengine.
Lengo la kutolewa Zakkatul Fitri
1.Kuwawezesha Waislam wasio kuwa na uwezo katika Siku hii kufurahi kama unavyofurahi wewe na Watu wako (Ahlubait)
2.Ibada
3.Zakaatul fitri hutolewa kwa ajili ya kusahihisha saum na hufidia ktk makosa madogo madogo
Zimepokewa hadithi tofauti katika Suala hili tuisome hadithi hii ya Ibn
Umar Radhi za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani Amesema "
Amefaradhisha Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani
Zakkah ya fitri (Ya kumalizika Ramadhani) Pishi ya Tende au Pishi ya
Shairi kwa Mtumwa na Huru (Muungwana), Mume na Mke, Mdogo na Mkubwa
katika Waislam, na akaamrisha (hiyo zakkah ya fitri) itolewe kabla ya
kutoka watu kuelekea katika Swalah (ya iddi).Kama alivyosema Mtume
hadithi hii imepokewa na Maimamu wawili Bukhari na Muslim.
KIASI KINA CHOTOLEWA CHA ZAKKATUL FITRI
Kwa Mujibu wa Hadithi tuliyo itanguliza ikiwa ni Pishi ya Chakula
Maarufu katika Mji uliopo inakuwa ni sawa na Kilo mbili na Gramu mia nne
(2.4 kg) takribani kwa nafaka kama mchele na mfano wake) ( au thamani
yake kwa baadhi ya wanachuoni )
Wenye kustahiki Zakkah hizi ni watu Maskini wasio na uwezo katika Waislam katika Sehemu Unayoishi.