Wasifu wa Al-HABIB UMAR BIN AHMAD BIN ABI-BAKAR BIN SUMAYT AL, radhi za Mwenyezi Mungu zimwalie.
Si
sisi wa kumweleza, hata ikasemwa kwamba kaelezwa. Letu sisi ni kurudi
kwa wale ambao wanatambulika kwamba wanaweza kumzungumza.Nasi tumeamua
kurudi kwa mwanazuoni wa wanazuoni wa zama zake na Bwana wa Msikiti Gofu
na Ukutani na naibu wa al-Habib Umar bin Ahmad bin Abi-bakar bin
Sumayt. Huyo ni Shaykh Sulayman bin Muhammad bin Said al-Alawy, radhi za
Mwenyezi Mungu zimwaalie yeye na ma-Shekhe zake. Kwenye ijaza ndefu,
anamwelezea hivi al-Habib:
“Na
nimepokea riwaya ya ilmu vilevile kutoka kwa Bwana wangu na nguzo
yangu, al-Habib, mwingi wa kuvumilia, mkuu aliyefika mbali kwenye ilmu,
Imam, al-Allaama mtukufu, machomozo ya nuru za uwongofu, kiongozi wa
ma-Imamu, na mwenye kuondosha mbabaiko, aliyekusanya ilmu za ndani na za
nje mwenye wajihi unaopendeza, aliyetakasika na sifa zote chafu, mwenye
akili inayowaka, Bwana wetu, Qutb, Umar bin Ahmad bin Sumayt al-Alawi
radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie. Nimemsahibu na nikatakhalaki kwa
khuluka zake na mengine yake. Akanifanyia talqini ya dhikri. Na
akanivisha na akanifanyia musaafaha na mushaabakah. Na ilbasi ilikuwa
kwa juba la baba yake, Mwenyezi Mungu amrehemu. Na tena akanipa ijaza
katika hayo. Na ningali bado nikienda kwake na yeye huyapamba masikio
yangu kwa johari za hikma na hakika za irfaani njema kweli, ambazo ni
nadra mtu kuzipata ama kuzisikia kwa asiokuwa yeye. Na kutoka kwake
nimepokea riwaya ya baadhi ya kitabu cha al-Ihyaa kwa kusikiza na mimi
kusoma mbele yake. Na vile vile baadhi ya vitabu vya ma-Bwana wakuu na
vitabu vya ma-Bwana wa Bani Alawi. Na nimesoma kwake baadhi ya kitabu
cha Tajriid as-Sahiih cha Hadithi. Akanipa ijaza kwenye vitabu
thalathini na kitu vya fiqhi.”
No comments:
Post a Comment