Sunday, September 08, 2013

WANASCOUT WA QIBLATEN SCHOOL WAWAFARIJI MAYATIMA.




Tarehe 31/08/2013 wanaskaut wa shule ya Qiblatain English Midium Primary School waliwatembelea yatima wanao lelewa katika kituo cha hisani kilichopo mbagala maji matitu,manispaa ya Temeke Dar es salaam.
Viongozi wa Qiblatain Skaut na wanaskauti wenyewe kwa pamoja walishiriki kuwafariji yatima hao kwa kuwapa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula,nguo,vinywaji,vitabu,madawa na Pesa taslimu Shilingi laki mbili na elfu sita.

Kwa mujibu wa kiongozi wa wana skaut wa Qiblatain mwalimu Omar Mavula amesema ni “utamaduni wa shule hii kufanya mambo ya kijamii mara kwa mara,mbali ya malengo mengine ya kuwafariji walengwa lakini pia tunafanya haya kwa lengo la kuwajenga watoto wetu wawe na moyo wa uzalendo na huruma kwa jamii yenye shida mbalimbali,na kwa hili tumefanikiwa kwani hivi vitu vyote unavyoviona hapa wamenunua wanafunzi wenyewe”alisema.

PICHA ZIFUATAZO ZINATOA TASWIRA HALISI YA TUKIO ZIMA LILIVYOKUWA.
 
HIVI NI VITU MBALIMBALI VILIVYOKUSANYWA NA WAN SKAUT WA QIBLATAIN VIKIWA TAYARI KWA SAFARI YA KUELEKEA MBAGALA MAJI MATITU KWA AJILI YA KUWAFARIJI MAYATIMA.

HAPA WANASKAUT WA QIBLATAIN WAKIINGIZA MIZIGO TAYARI KWA SAFARI.

 HAPA WANASKAUT WAKIKABIDHI ZAWADI.

"WEWE NI NDUGU YANGU,NIPO PAMOJA NA WEWE,USIHUZUNIKE EEE"NDIVYO ANAVYOONEKANA KUSEMA MWANAFUNZI ASIA RAMADHAN KWANGAYA KUTOKA QIBLATAIN SCHOOL.

WANASKAUT WA QIBLATAIN WAKIWA WAMECHANGANYIKA NA WALENGWA 

"NYAMAZA NDUGU YANGU,USILIE,TUMEKUJA HAPA KWA AJILI YENU"NDIVYO ANAVYOONEKANA MWANAFUNZI WA QIBLATEN AKIWA AMEMBEBA MTOTO YATIMA.

"NDUGU ZETU,JAPO TULIVYOLETA NI VICHACHE LAKINI HII SABUNI ITAWASAIDIA KIDOGO,NAOMBA MUIPOKEE",NDIVYO ALIVYOWAAMBIA MWANAFUNZI HUYO WA QIBLATEN WAKATI AKIWAKABIDHI MAYATIMA HAO MSAADA WA VITU MBALIMBALI.

No comments:

Post a Comment