Na Salva Rweyemamu, Mwanza
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumapili, Septemba 8, 2013, amezindua mtambo wa kufua umeme kiasi
cha megawati 60 katika eneo la Nyakato mjini Mwanza, umeme ambao
utachangia kwa kiwango kikubwa kupunguza shida ya umeme katika Mkoa wa
Mwanza na mikoa ya jirani.
Aidha,
Rais Kikwete ameiangiza Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) kuanza mara moja maandalizi ya kupeleka umeme kwenye
machimbo ya madini ya nikeli yaliyoko Kabanga, Ngara, Mkoa wa Kagera.
Vile
vile, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali yake itaharakisha mipango ya
kujenga reli hadi kwenye eneo hilo kama maandalizi ya kuanza kuchimbwa
kwa madini hayo ambayo ni mazito na kuyasafirisha kwa barabara kwenda
bandarini Dar Es Salaam kutaharibu kwa haraka barabara zinazojengwa kwa
gharama kubwa nchini.
Akizungumza
kabla ya kuzindua mtambo huo, Rais Kikwete ameitaka Wizara ya Nishati
na Madini kuharakisha mipango ya kuunganisha eneo la Kabanga, Ngara,
Mkoani Kagera kwenye Gridi ya Taifa ili uzalishaji wa madini ya nikeli
usije kukwamishwa na ukosefu wa umeme. Amesema kuwa mgodi huo utahitaji
umeme mwingi kiasi cha megawati 40.
Rais
amesema kuwa Serikali yake itahakikisha inafikisha reli kwenye eneo la
Kabanga mapema ili kuhakikisha kuwa nikeli inayozalishwa inasafirishwa
kwa reli badala ya barabara. Amesema kuwa madini hayo ni mazito mno na
kuyasafirishwa kwa barabara kutaharibu kabisa na katika muda mfupi
barabara ambazo zinajengwa nchini kwa gharama kubwa.
Mtambo
wa Umeme wa Nyakato wenye uwezo wa kuzalisha megawati 60 ulianza
kujengwa mwaka jana, 2012, baada ya Serikali ya Tanzania kutiliana
mkataba wa ujenzi na Kampuni ya Semco and Rolls Royce ya Norway mwaka
2011 wakati maandalizi ya ujenzi huo yalipoanza.
Gharama
za ujenzi wa mtambo huo ambazo ni sh bilioni 130 (Euro milioni 48.7 na
dola za Marekani 15.9) zimelipwa kwa asilimia 100 na Serikali ya
Tanzania.
Akizungumza
na wananchi kwenye sherehe ya uzinduzi huo, Rais Kikwete amesema kuwa
umeme siyo anasa bali ni moja ya vigezo vya msingi na muhimu kabisa vya
maendeleo.
“Vipo
vigezo vingi vya maendeleo ya nchi na binadamu, lakini moja ya vigezo
hiyo ni umeme. Na ukiangalia matumizi ya umeme kwa kila nchi yanaonyesha
kiwango cha maendeleo cha nchi hiyo. Katika Marekani, kwa mfano, kila
mwananchi anatumia kiasi cha kilowati 12,000 kwa wastani. Sisi katika
Tanzania ni kilowati 89 tu na wastani wa Bara la Afrika ni kilowati
150,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Nc
hi yetu ya Tanzania ina umeme kiasi cha megwati 1,450 tu wakati katika
Afrika Kusini ni megawati 45,000 na unaweza kuona tofauti ya maendeleo.
Hivyo, ni muhimu sana kwetu kuongeza kiwango cha kuzalisha umeme katika
nchi yetu.”
Katika
siku ya tatu ya ziara yake kukagua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa
Mwanza, Rais Kiwete pia amefungua Kituo cha Polisi cha Nyakato ambacho
kimegharimu sh milioni 450, Serikali ikiwa imechangia kiasi cha asilimia
20 cha gharama hizo.
Kituo
hicho cha kisasa kilianza kujengwa mwaka 2003 lakini ujenzi wake ukawa
unakwamakwama kutokana na ukosefu wa bajeti hadi uongozi wa polisi wa
Mkoa wa Mwanza ulipoamua kukijenga kituo hicho kwa njia ya
kuishirikisha jamii na ikaundwa Kamati ya Ujenzi chini ya uenyekiti wa
Bwana Alfred Wambiura.
Akizungumza
kwenye sherehe ya ufunguzi wa kituo hicho, Rais Kikwete ameahidi kuwa
atajenga nyuma moja kwa ajili ya mkazi ya polisi. Kituo hicho kina jumla
ya askari polisi 65.
No comments:
Post a Comment